Na Barnabas Kisengi Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amewaongoza menejimenti na wafanyakazi wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Katibu Mkuu mpya Bw. Anderson Mutatembwa aliyeapishwa jana Ikulu. Aidha Katibu Mkuu Dkt. Abbasi amewaongoza wafanyakazi hao kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Bw. Juma Selemani Mkomi aliyeapishwa jana kuwa Katibu Mkuu-Ofisi
Na Barnabas Kisengi Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amewaongoza menejimenti na wafanyakazi wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Katibu Mkuu mpya Bw. Anderson Mutatembwa aliyeapishwa jana Ikulu.
Aidha Katibu Mkuu Dkt. Abbasi amewaongoza wafanyakazi hao kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Bw. Juma Selemani Mkomi aliyeapishwa jana kuwa Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais Utumishi.
“Leo tunapokutana hapa kumuaga Bw. Mkomi na kumkaribisha Bw. Mutatembwa labda mfahamu tu sisi watatu hapa tunafahamiana siku nyingi na kubwa wote tulikuwa katika Timu iliyoratibu kwa mafanikio makubwa ushiriki wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika filamu ya Royal Tour na sote tulizunguka naye Mhe Rais nchi nzima kwa hiyo tunaufahamu mkubwa wa jinsi ya kuutangaza utalii kwa kiwango kikubwa,” amesema Dkt. Abbasi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Mkomi amewashukuru wafanyakazi hao kwa ushirikiano mkubwa waliompa akiwa Wizarani hapo huku Bw. Mutatembwa naye akiahidi kujifunza haraka ili kazi iendelee na kuomba ushirikiano wa wafanyakazi wote.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *