Rais Dkt. Mwinyi amezungumza na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Khalifa Abdulrahman Almarzouqi.

Rais Dkt. Mwinyi amezungumza na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Khalifa Abdulrahman Almarzouqi.

STATE HOUSE ZANZIBAROFFICE OF THE PRESS SECRETARYPRESS RELEASEZanzibar Disemba, 2020 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. HusseinAli Mwinyi amewaomba Wawekezaji kutoka nchi za Jumuiya yaKiarabu (UAE) kuja kuwekeza nchini, hususan katika sekta ya Utalii. Dk. Mwinyi ametoa wito huo leo Ikulu Jijini Zanzibar, wakati alipokuwa namazungumzo na Balozi wa Falme za

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar Disemba, 2020

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi amewaomba Wawekezaji kutoka nchi za Jumuiya ya
Kiarabu (UAE) kuja kuwekeza nchini, hususan katika sekta ya Utalii.

Dk. Mwinyi ametoa wito huo leo Ikulu Jijini Zanzibar, wakati alipokuwa na
mazungumzo na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Khalifa
Abdulrahman Almarzouqi, aliefika kujitambulisha kwa Rais.

Alisema katika dhana ya kuimarisha uchumi, Zanzibar inalenga
kuimarisha uchumi wake kupitia Uchumi wa Buluu, hivyo inahitaji
Wawekezaji kutoka mataifa mbali mbali Duniani, ikiwemo UAE ili kuwekeza
kupitia sekta ya Utalii yenye vivutio mbali mbali katika visiwa vya Unguja na
Pemba.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalenga kukifanya kisiwa cha
Pemba kuwa eneo muhimu la Uwekezaji, hivyo akawataka wawekezaji
kutoka nchi hizo kuja kuwekeza katika miradi mbali mbali.

Alisema sheria za Uwekezaji , ikihusisha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya
miradi mbali mbali zinatoa fursa kwa Wawekezaji kuwekeza katika maeneo
mbali mbali yakiwemo ya visiwa.

Aidha, Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa nchi za Jumuiya hiyo kwa uhusiano
na ushirikiano mzuri na wa muda mrefu kati yake na Zanzibar, pamoja na
misaada mbali mbali inayoendelea kutolewa kupitia nyanja mbali mbali za
kiuchumi na kijamii.
A

lisema nchi za Jumuiya ya Kiarabu zimekuwa zikiunga mkono juhudi za
serikali na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi
na kijamii ya Zanzibar, ambapo kwa nyakati tofauti zimesaidia miradi mbali,ukiwemo Mfuko wa ‘Khalifa Fund’ unaolenga kuwawezesha kiuchumi
Vijana wa Zanzibar.

Vile vile aliziomba taasisi na wadau wa maendeleo kutoka nchi hizo
kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuuweka katika mazingira
bora zaidi Mji Mkongwe wa Zanzibar, (ulio katika Urithi wa Ulimwengu) ili
uweze kuwa eneo la kiuchumi.

Nae, Balozi wa UAE nchini Tanzania Khalifa Abdulrahman Almarzouqi
alimshakikishia Rais Dk. Mwinyi kuwa UAE itaendeleza uhusiano na
ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Zanzibar, sambamba na kuendelea
kuisaidia nchi hiyo katika nyanja za Kiuchumi na kijamii.

Aidha, aliahidi kuwashajiisha Wawekezaji wa nchi hizo kuja nchini
kuwekeza, akibainisha kuwepo kwa kampuni mbali mbali zinazowekeza
katika sekta ya utalii kupitia miradi mbali mbali, ikiwemo ya ujenzi wa Hoteli
kubwa za kitalii, michezo ya baharini na miradi mingineyo.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822
E-mail: abdya062@gmail.com

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »