Fountain Gate Academy yatoa Ufafanuzi wa Utata wa Shilingi Milioni 200 walizopatiwa baada ya ushindi wa Mashindano ya Sekondari Africa Mashariki (CECAF)

Fountain Gate Academy yatoa Ufafanuzi wa Utata wa Shilingi Milioni 200 walizopatiwa baada ya ushindi wa Mashindano ya Sekondari Africa Mashariki (CECAF)

Na Moreen Rojas Dodoma Mkurugenzi wa fountain gate academy Japhet Makau ametoa ufafanuzi kwa kile kinachoendelea mtaani na kwa wazazi kuhusu Shilingi milioni 200 walizoshinda kwenye mashindano ya shule sekondari afrika mashariki CECAFA.Makau ametoa ufafanuzi huo katika ofisi kuu za fountain academy zilizopo wajenzi jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo likiwa

Na Moreen Rojas Dodoma


Mkurugenzi wa fountain gate academy Japhet Makau ametoa ufafanuzi kwa kile kinachoendelea mtaani na kwa wazazi kuhusu Shilingi milioni 200 walizoshinda kwenye mashindano ya shule sekondari afrika mashariki CECAFA.
Makau ametoa ufafanuzi huo katika ofisi kuu za fountain academy zilizopo wajenzi jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo likiwa ni kuwatoa hofu wazazi wa wanafunzi hao walioshiriki mashindano hayo.


Aidha Makau amesema amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa wazazi wakitaka watoto wao wagawiwe fedha hizo walizoshinda wakati huo wenyewe wamepewa masharti ya kwamba fedha hizo zinatakiwa kuingizwa kwenye miradi maalum kwa lengo la kuendeleza michezo.
“Fedha hizi tumepewa kwa ajili ya matumizi ya project mbalimbali zinazohusiana na michezo kama vile kununua uwanja mkubwa wenye hadhi pamoja na kujenga nyumba za kulala kwa ajili ya wanafunzi wetu wa kike”Amesisitiza Makau


Mkurugenzi Makau amewasihi wazazi kuacha kusikiliza mameno ya watu na badala yake kusikiliza ufafanuzi huu na kuhusu mchanganua wa hela kwani toka kuanzishwa kwa mashindano hayo kama taasisi imekuwa ikitumia fedha nyingi kujiandaa kama timu hadi kufikia finali na kuchukua ubigwa.
” Sijambo rahisi kwa wazazi kuelewa namna ambavyo fedha hizi zinapaswa kutumika lakini niwatoe hofu kwamba kila kitu kipo sawaa zaidi waendelee kutoa sapoti kwa watoto haswa wa kike wenye vipaji ili kuendelea kukuza vipaji na uzuri soka la wanawake linakuwa na linafanya vizuri”Amesisitiza Makau


Makau amesema Kwa uwezo tulionyesha kwenye mashindano hayo tumeweza kupata fursa ya kupeleka timu yetu nje ya nchi na licha ya vijana wangu kuzidiwa maumbile na timu zingine za afrika kama vile Uganda lakini walionyesha uwezo wa hali ya juu na sasa afrika na dunia wameweza kutambua fountain ni kina nani na perfomance yetu ikoje uwanjani.
Fountain gate academy ndio washindi wa mashindano ya shule za sekondari afrika mashariki CECAFA ambapo ushindi huo ulipatikana kwa fountain kuichapa Rwanda mabao 3 kwa 0 katika uwanja wa chamazi Azam mbagala Jijini Dar es salaam.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »