TPHPA Yadhibiti Ndege aina ya Kweleakwelea Milioni 227.4 na kuokoa Tani 1056.3 za Mazao ya Nafaka

TPHPA Yadhibiti Ndege aina ya Kweleakwelea Milioni 227.4 na kuokoa Tani 1056.3 za Mazao ya Nafaka

Na Moreen Rojas Dodoma Mamlaka ya afya ya mimea na viatilifu Tanzania TPHPA imefanikiwa kudhibiti ndege aina ya kweleakwelea milioni 227.4 na kufanikiwa kuokoa Tani 1056.3 za mazao ya nafaka.Prof.Joseph Ndunguru amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kueleza utekelezaji wa majukumu ya mimea na viatilifu nchini Tanzania. Aidha Prof Joseph amesema

Na Moreen Rojas Dodoma


Mamlaka ya afya ya mimea na viatilifu Tanzania TPHPA imefanikiwa kudhibiti ndege aina ya kweleakwelea milioni 227.4 na kufanikiwa kuokoa Tani 1056.3 za mazao ya nafaka.
Prof.Joseph Ndunguru amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kueleza utekelezaji wa majukumu ya mimea na viatilifu nchini Tanzania.

Aidha Prof Joseph amesema udhibiti huu umefanyika katika Mikoa ya Tabora katika wilaya ya Uyui na Igunga,Kigoma wilaya ya Kibondo,Geita wilaya ya Geita,Shinyanga Katika wilaya ya ya Shinyanga vijijini na kishapu, Mwanza wilaya ya Sengerema,Mbeya wilaya ya Mbarali,Pwani  Wilaya ya Chalinze, Arusha  wilaya ya Arumeru na Simanjiro, Manyara wilaya ya Babati, Kilimanjaro wilaya ya Same na Moshi  kwa kutumia ndege maalumu kutoka shirika la kilimo na chakula duniani (FAO) na ndege nyingine kutoka shirika la kuthibiti.
“Mamlaka imekagua tani 5,343,380.59 za mazao ya nafaka,bustani,mizizi,mbegu za mafuta katika vituo vya mipakani,bandari na viwanja vya ndege ambapo jumla ya vyeti 29,033 vya usafi wa mimea kwa ajili ya kuruhusu mazao kusafirishwa nje ya nchi na vyeti 3359 vya kuruhusu mazao kuingia nchini vimetolewa”Amesema Prof.Ndunguru


Aidha amesema mamlaka imedhibiti milipiko ya panya katika mikoa mbalimbali,jumla ya eneo la ekari 122,190 lililokolewa na uvamizi wa panya,mafunzo ya namna ya kuwatambua aina ya panya na mbinu za kudhibiti yalitolewa.
Amesema kuwa jumla ya wakulima 2987 na maafisa ugani 16 katika kata 16 za halmashauri ya wilaya ya kilombero,mafunzo ya mbinu za kudhibiti nzi wa matunda kwa wakulima 849 na maafisa ugani 7 katika wilaya ya Handeni katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka februari 2023.


Prof Ndunguru amesema tumetoa elimu kwa wakulima namna ya kudhibiti viatilifu na kufanya ukaguzi wa mazao na vipande ili kuweza kuuza mazao ndani ya nchi na nje ya nchi.
Aidha amesema mamlaka imefanikiwa kusajili jumla ya wadudu rafiki aina 11 ambapo matumuzi ya wadudu rafiki husaidia kupunguza matumizi ya viuatilifu vya viwandani 
Amesema kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kudhibiti nzige wekundu(IRLCO_CSA) mamlaka imefanya ufuatiliaji kwenye mazalia ya asili ya nzige wekundu.
“Jumla ya hekta 195,150 zilifanyiwa ufuatiliaji kwa njia ya anga kwa kutumia helikopta na kubaini hekta 1,000 zilizokuwa na kiwango kikubwa cha nzige”

Sanjari na hayo mamlaka inakabiliwa na changamoto ya uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viatilifu,elimu juu ya visumbufu na namna ya kudhibiti.
“Katika eneo hili nawaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zenu vizuri juu ya taarifa hizi kwa wakulima,kwa upande wetu kama taasisi tunajitahidi kutoa elimu kwa wakulima kupitia shamba darasa na vikao vya kijiji lakini pia tunatumia chanel yetu ya taasisi ili kufikisha ujumbe kwa wakulima na kufuata njia bora za kisasa ili kuleta matokeo chanya kwa mkulima”Amesisitiza Prof.Ndunguru
Aidha Porf Ndunguru ametoa Rai kwa wakulima kuwa makini na viatilifu vya nje ya nchi kwani kumekuwepo na wauzaji wa viatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »