CHONGOLO: TANZANIA INAKOPA KWA AJILI YA MAENDELEO, TUSIPOTOSHWE

CHONGOLO: TANZANIA INAKOPA KWA AJILI YA MAENDELEO, TUSIPOTOSHWE

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amesema Tanzania haina mzigo wa Madeni kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki, tuwapuuze watu wanaobeza mpango wa Serikali kukopa Fedha Nje ya Nchi, kwani hatua ya Serikali kukopa ni kuendelea Kuijenga Tanzania ili iwe imara Kiuchumi kama ilivyo kwa mataifa yaliyopiga hatua Kimaendeleo.

Katibu Mkuu Chongolo amebainisha hayo leo Machi 01, 2023 Katika Kijiji cha Ulemo, Wilaya ya Iramba ikiwa ni Siku ya Tatu ya Ziara yake mkoani Singida.

Amesema Tanzania sio nchi ya kwanza kukopa Fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya Wananchi wake, kwani hata mataifa makubwa kama Marekani nayo hukopa Fedha pale inapobidi ili kuweka Sawa mambo yake na hulipa madeni yake pole pole.

“Wapo watu kila wakisimama wanasema Tanzania inakopa sana, na wanakaza nyuso na Shingo zao ili kuwaaminisha hilo, ngoja niwaambie katika nchi za Afrika Mashariki Taifa ambalo halina mzigo wa mkopo ni Tanzania” amesema Chongolo.

Ameongeza kuwa kinachotokea ni kwamba Serikali hupanga mipango yake na kuitekeleza kwa namna ilivyopanga kwa ajili ya maendeleo ya wote, huku akiwataka Watanzania kutodanganyika na aina yoyote ya uongo unaosambazwa na watu hao kuhusiana na Serikali kuendelea kukopa Fedha nje ya nchi.

Kwa Upande wake Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Sophia Mjema, amewaasa viongozi wa Chama hicho katika ngazi zote, kuendelea kueneza Sera za CCM kwa Vitendo ikiwa ni pamoja na kuweza kuisemea na kuisimamia Miradi inayofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo yupo mkoani Singida kwa ziara inayolenga kukagua Utekelezaji wa Ilani Uchaguzi ya Chama hicho, kukagua Uhai wa CCM kuanzia ngazi ya Shina pamoja na kuzungumza na makundi mbalimbali ya Kijamii.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »