NAIBU NDEJEMBI WAZIRI ATOA MIEZI MIWILI KUKAMILIKA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA SINGIDA

NAIBU NDEJEMBI WAZIRI ATOA MIEZI MIWILI KUKAMILIKA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA SINGIDA

Na Barnabas Kisengi Singida Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa miezi miwili  kwa Mkurungenzi wa Halmashauri ya Manyoni kukamilisha ujenzi miundombinu yote ya shule maalum ya Sayansi ya Wasichana ya Mkoa wa Singida. Ndejembi Ametoa maagizo hayo Machi, 01 2023 wakati alipofanya ziara ya

Na Barnabas Kisengi Singida


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa miezi miwili  kwa Mkurungenzi wa Halmashauri ya Manyoni kukamilisha ujenzi miundombinu yote ya shule maalum ya Sayansi ya Wasichana ya Mkoa wa Singida.


Ndejembi Ametoa maagizo hayo Machi, 01 2023 wakati alipofanya ziara ya kukagua shule ya sayansi ya kidato cha kwanza hadi cha sita inayojengwa Solya Wilaya ya Manyoni kwa gharama ya  shilingi bilioni 3.
Naibu waziri Ndejembi amebaini mapungufu mengi katika usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni pamoja na kutofuatwa mwongozo wa manunuzi na taratibu za malipo kwa Makandarasi wanaoendelea na ujenzi.


Amemuagiza Afisa wa TAKUKURU wilaya ya Manyoni  ndani ya siku saba kufanya uchunguzi na kuwasilisha taarifa yake ya Uchunguzi katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI juu mapungufu aliyoyabaini katika ujenzi wa shule hiyo ili hatua sitahiki zichukuliwe.


Aidha Naibu waziri Ndejembi amemuagiza Mkurungenzi wa Halmashauri ya wilaya ya manyoni kuwachukulia hatua za kinidhamu afisa manunuzi na mhandisi kwa kufanya malipo kwa mkandarasi kinyume na taratibu ambapo malipo yalifanyika kabla ya kibali cha malipo kutolewa pomoja kununua vifaa zaidi ya BQ iliyoelekeza.


Ndejembi amesema RAIS Dkt SAMIA SULUH HASSAN  mwezi Januari, 2022 alitoa bilioni 3 za awamu ya kwanza  kujenga shule hiyo ambayo ilitakiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022 na kuanza kupokea wanafunzi mwezi Januari mwaka huu lakini mpaka sasa ujenzi haujakamilika.

Mkoa wa Singida ni moja kati ya mikoa kumi nchini iliyopokea  kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za wasichana za mikoa ili kujenga vyumba vya madarasa 12, jengo la utawala 1, maabara 4, maktaba 1, matundu ya vyoo 16, chumba cha jenereta, bwalo, mabweni 5, mitaro ya maji, kichomea taka, matanki ya chini ya maji, matanki ya plastiki, uzio, njia za kutembelea na nyumba mbili za walimu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »