NAIBU WAZIRI MAVUNDE AELEZA MKAKATI WA SERIKALI KUBORESHA KITUO CHA UTAFITI ZAO LA MICHIKICHI-KIGOMA

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AELEZA MKAKATI WA SERIKALI KUBORESHA KITUO CHA UTAFITI ZAO LA MICHIKICHI-KIGOMA

Na Mwandishi Wetu Kigoma Naibu Waziri wa Kilimo,  Anthony Mavunde ameeleza mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya kilimo wa kukiboresha kituo cha utafiti wa Kilimo-TARI KIHINGA ili kisaidie kuchochea maendeleo ya zao la Mchikichi.  Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo mkoani Kigoma alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kigoma wakati ziara ya Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri

Na Mwandishi Wetu Kigoma


Naibu Waziri wa Kilimo,  Anthony Mavunde ameeleza mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya kilimo wa kukiboresha kituo cha utafiti wa Kilimo-TARI KIHINGA ili kisaidie kuchochea maendeleo ya zao la Mchikichi. 


Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo mkoani Kigoma alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kigoma wakati ziara ya Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutathmini maendeleo ya zao la michikichi nchini.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, ili kutekeleza mpango wa uzalishaji bora wa mbegu za Michikichi uweze kueleta matokeo bora na makubwa zaidi.…Katika Bajeti inayokuja Serikali inaendelea kutenga fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya kituo cha Utafiti cha TARI – KIHINGA kuwa cha kisasa kwa kuwa na miundombinu bora na kuongeza uzalishaji wa miche ya michikichi.


Pamoja na hayo pia tumekipatia kituo hichi Shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi,maabara na nyumba za watumishi,ukiwemopia mpango wa kuwajengea uwezo watafiti wa zao hili la mchikichi kwa kuwapeleka masomoni na kujifunza katika maeneo ambayo yamefanya vizuri zaidi.


Katika kuzijengea uwezo Taasisi zinazo husika na Uzalishaji wa Miche ya Michikichi pamoja na kuboresha usimamizi wa uzalishaji huo  tunashauri kwamba fedha zinazotengwa na Halmashauri kwajili ya usimamizi wa Miche ya michikichi, zielekezwe pia kwenye Taasisi kubwa zinazo zalisha Miche ya Michikichi, Taasisi hizo ni kama vile, JKT Bulombora, Gereza la Kwitanga pamoja na TARI, ili kuzijengea uwezo Taasisi hizo wa uzalishaji wa Miche hiyo, na baadae kuleta Tija. 

Uzalishaji  wa miche bora aina ya TENERA utaenda sambamba na kuwaunganisha wakulima wadogo pamoja na vikundi vya wanawake na SIDO ili waweze kupata mitambo rahisi ya uchakataji wa mafuta ya mawese na kujiongezea kipato kupitia benki ya maendeleo ya kilimo (TADB)ambayo mpaka sasa imeidhinisha kiasi cha Tsh *1,400,000,000* kwa ajili kuchochea shughuli za uongezaji thamani wa zao la mchikichi”Alisema Mavunde


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye amesema kwamba mwamko wa wananchi kulima zao la mchikichi ni mkubwa na mahitaji ya miche bora pia ni makubwa hivyo juhudi ya wizara kilimo ya kukiongezea uwezo kituo cha TARI-KIHINGA itakuwa ni hatua kubwa ya maendeleo ya zao la mchikichi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »