Alhaji Kimbisa Awataka Viongozi CCM kufanya Mikutano

Alhaji Kimbisa Awataka Viongozi CCM kufanya Mikutano

Na Barnabas Kisengi Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma CCM Alhaji ADAM KIMBISA ameitaka kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani kuhakikisha inasima na kuhakikisha viongozi wa cha na Serikali wanafanya mikutano ya adhara kwa Wananchi naekuwaekeza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na RAIS

Na Barnabas Kisengi Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma CCM Alhaji ADAM KIMBISA ameitaka kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani kuhakikisha inasima na kuhakikisha viongozi wa cha na Serikali wanafanya mikutano ya adhara kwa Wananchi naekuwaekeza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na RAIS Dkt SAMIA SULUH HASSAN.


Kauli hiyo imetolewa Machi 03 2023 na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma Alhaji Adamu Kimbisa alipokutana na Wajumbe wa kamati ya Siasa kata ya kilimani jijini Dodoma wakati wakijadili mikakati ya kuimarisha Cha Cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya shina,tawi,kata,wilaya hadi Mkoa kuelekea chaguzi zijazo za wenyeviti wa Serikali za Mitaa mwakani na kufuatiwa na Uchaguzi Mkuu 2025 wa madiwani,wabunge na RAIS.
“Niwaeleze Ukweli mwaka 2020 mkoa wa dodoma hatukufanya vizuri hasa wilaya ya dodoma Mjini katika kura za Mhe RAIS hivyo nimewaita hapa tujiwekee mikakati ya kuimarisha Chama na kuhakikisha kuanzia Sasa tunajipanga vizuri katika chaguzi za mwakani za Wenyevyiti wa Serikali za Mitaa  hivyo lazima tuanze kujipanga mapema kwa wanachama wetu” amesema Alhaji Kimbisa


Aidha Alhaji Kimbisa akawashukia Diwani wa kata ya kilimani Neema Mwaluko na katibu wa CCM kata ya kilimani kuhakikiaha wanavuja makundi yao ya uchaguzi wa 2020 na 2022 ili waweza kufanya kazi kama timu moja ya kukijenga Chama cha Mapinduzi hasa kata ya kilimani kwakuwa kata ya kilimani ndio kata kubwa iliyobeba viongozi wengi wakubwa wa serikali na Chama.
“Nafahamu tangu nimeanza kusikiliza vikao hivi vya kamati za siasa malalamiko mengi ya kutoka elewana ni Diwani na katibu hivyo muwe makini maana kikao cha mwisho cha kuwajadili ni kikao changu cha mkoa hivyo msitegemee mtafika mbali hapa kwangu Ndio Mwisho wenu na tukiangalia wote ni wa CCM Sasa magomvi ya Nini” amesema Alhaji Kimbisa


Nafahamu kuwa Diwani ukiitwa kwenye vikao huendi hujui kamati ya siasa ni chombo kikubwa Sasa kwenye kata yako pia hamfanyi mikutano ya wanachi kuwaekeza Juu ya Chama na serikali imefanya nini hivyo nawaagiza hakikisheni mnavunja makundi na kufanya mikutano kwa wananchi ili watambue Serikali ya awamu ya sita imefanya nini kuwaletea maendeleo.


Alhaji Kimbisa pia ameiagiza kamati ya siasa ya kata kuhakikiaha inaongeza idadi ya wanachama kwakuwa idadi iliyopo hairidhishi kabisa kama mnaniambia kata ina zaidi ya watu elfu 9,000 na hadi Sasa mnaeanachama elfu 1,800 ni sawa naeasilimia 19 hii bado ni ndogo sana sasa hakikisheni mnafanya vikao na kuwashawishi Wananchi kuwa na kadi za CCM.


Mhe Diwani hakikisha unafanya mikutano na kukamilisha ahadi mlizowaahidi Wananchi kwenye kata hii itatatujengea imani kubwa kwa Wananchi wetu ambapo mwakani tusimamie nguvu kubwa kuwashawishi Wananchi hapo kila moja akitimiza wajibu wake tutafikiwa vizuri katikaechaguzi zijazo.


Aidha Alhaji Kimbisa amemwagiza Diwani wa kata ya kilimani kuhakikisha Jumatatu anafika Katika ofisi za Halimashauri ya Jiji la Dodoma kufuatilia nyaraka za maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za taasisi hata eneo lililotengwa kwa ajili ya shule ya secondary na eneo la wazi na msikitini ambayo amesema yamepitiwa na kivuko cha reli ya mwendo kasi viwanja vilivyobaki vimebaki kiasi gani na kwa matumizi gani na kuwasilisha taarifa hiyo kwa kamati ya Siasa ya kata na kwa makatibu CCM wilaya na Mkoa ili kuweza kujua utatuzi wa kupata eneo la Ujenzi wa secondary kutokana na kata hiyo kongwe kutokuwa na shule ya secondary tangu kuanzishwa kwa kata hiyo ya kilimani jijini Dodoma.

Kwa Upande wake katibu mkoa wa Dodoma CCM PILI MBAGA ameitaka kamati ya siasa kata kutambua majukumu yao na kuhakisha wanaongeza idadi ya wanachama na kushuka chini kwenye matawi na mashina kuhakikisha wanafanya vikao kwa wanachama ili kuweza kuimarisha Cha kuanzi ngazi ya chini
PILI MBAGA pia amewataka Viongozi wote kwa ujumla ambao Bado wanamakundi ya uchaguzi kuhakikisha wameyavunja na kuwa na kundi moja tu la CCM na kuendelea kuinadi na kuisimamia ilani ya chama Cha Mapinduzi na kuisimamia Utekelezaji wa ilani yetu.


Vikao hivi vya kamati ya siasa za kata na mwenyeki wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa ni vikao vya kuimarisha chama na kuchukua changamoto mbalimbali zilizopo Katika kata na kuzipatia ufumbuzi wa haraka Ili kujiandaa na chaguzi zijazo na changamoto kubwa inayojitokeza katika kata nyingi ni changamoto ya migogoro ya aridhi na kutokuwa na maelewano kati ya madiwa na Makatibu kata na vikoa hivi vya mwenyeki wa CCM Mkoa na kamati za siasa vineanzia Katika wilaya ya dodoma Mjini ambapo mwenyeki wa CCM Mkoa anaendelea kukutana na kamati za siasa kata zote 41 za Dodoma Mjini

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »