Wafanyakazi Wanawake DUWASA watoa misaada mbalimbali katika Shule ya Kigwe Vizuri Bahi

Wafanyakazi Wanawake DUWASA watoa misaada mbalimbali katika Shule ya Kigwe Vizuri Bahi

Na Barnabas Kisengi Bahi Dodoma Kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08. 2023 wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), wametoa msaada wa magodoro, sabuni, taulo za kike, mafuta na nguo katika shule ya Msingi ya Kingwe Viziwi iliyopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma. Wafanyakazi hao

Na Barnabas Kisengi Bahi Dodoma


Kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08. 2023 wafanyakazi wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), wametoa msaada wa magodoro, sabuni, taulo za kike, mafuta na nguo katika shule ya Msingi ya Kingwe Viziwi iliyopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.


Wafanyakazi hao wa DUWASA Wanawake  wametoa wito kwa wazazi na walezi kutowaficha nyumbani watoto wenye ulemavu na pia kuwaomba mashirika, taasisi na watu binafsi kusaidia shule hiyo.


Katibu wa Wafanyakazi Wanawake wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA Bi Esther Mlewa amesema hayo Machi 4, 2023 wakati wakitoa msaada wenye thamani ya Sh. Milioni moja na mahitaji mbalimbali katika shule hiyo.
“Wanawake tumeguswa na changamoto zilizopo kwenye shule hii na kuamua kutoa misaada kwa sababu sisi ni wazazi na shule hii ina wanafunzi wenye mahitaji, maalumu” Amesema Bi Esther Mlewa.


Aidha katibu wa Wafanyakazi Wanawake wa wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA amesema wamekuwa wakifanya hivyo  kila mwaka katika wilaya mbalimbali zilizopo mkoa wa Dodoma na wataendelea kutoa misaada hiyo kwa lengo la kuwapa faraja watoto hao na kutambua kuwa kuna watu wanaupendo kwao.


Awali, Afisa Elimu maalum wilaya ya Bahi, Sarah Chizingwa amewasihi wazazi kutowaficha watoto wenye ulemavu kwakuwa suala hilo sio adhabu na wanahitaji kupata elimu kama wengine.
“Kuwa na mtoto mlemavu sio adhabu hivyo tuwasihi wawalete kwenye shule maalum za viziwi, tuwashauri kwa upendo unaohitajika kama wengine ambao hawana uziwi,” amesema Sarah.


Aidha, amesema ulinzi na usalama kwa watoto wenye uziwi unahitajika kwakuwa wana changamoto wasiachwe wakazagaa hovyo barabarani au mitaani.


Diwani wa Kata ya Kigwe, Adon Mabalwe amewataka wazazi wa kike kuwa na utaratibu wa kuja katika shule hiyo kuzungumza na wanafunzi wa kike kwakuwa huwa wanapitia changamoto ambazo wanakosa watu wa kuzungumza nao.


Akisoma risala kuhusu shule hiyo, Mwalimu Mkuu Thadei Mwagila amesema shule ina wanafunzi 112 kati ya hao 67 ni wanawake na 45 wanaume.


Amesema shule hiyo haipo nyuma kitaaluma ikilinganishwa na miaka ya nyuma na inajihusisha na shughuli za uzalishaji mali.
Amefafanua shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vifaa vya kufundishia somo la Tehama, upungufu wa walezi upande wa mabweni ya wavulana.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »