Watoto Wanatakiwa kusajiliwa kujiunga na Bima za Afya kupita Shule wanazosoma.

Watoto Wanatakiwa kusajiliwa kujiunga na Bima za Afya kupita Shule wanazosoma.

Na Barnabas Kisengi Dodoma Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wa Taifa (NHIF)umewashauri wazazi na walezi kuwasajili watoto wao kama wategemezi wao kwenye bima ya afya au kuwasajili kupitia shule wanazosoma. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Benard Konga ametoa kauli hiyo Machi 14. 2023 Jijini Dodoma wakati Akizungumza na

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wa Taifa (NHIF)umewashauri wazazi na walezi kuwasajili watoto wao kama wategemezi wao kwenye bima ya afya au kuwasajili kupitia shule wanazosoma.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Benard Konga ametoa kauli hiyo Machi 14. 2023 Jijini Dodoma wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maboresho Katika utaratibu wa usajili wa watoto kupitia Mpango wa Toto Afya Kadi.
Konga amesema kuwa lengo la kufanya hivyo  ni kuongeza wigo wa wanachama Katika mfumo wa Bima ya afya kuelekea bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanachama Katika makundi hayo wanajiunga kama Familia au kaya  ya wanafunzi kupitia shule wanazosoma.


“Mpango wa Toto Afya Kadi ulianza rasmi  Mwaka 2016 baada ya kufanyiwa upembuzi na lengo ikiwa ni kuwajumuisha watoto kupitia shule zao,”Amesema konga
Aidha amebainisha kuwa  nia ikiwa ni kufikia kundi kubwa la watoto walio chini ya umri wa miaka18 ambao kitakwimu  ni zaidi ya nusu ya Wananchi wote Ili kufikia azma ya serikali ya watu wote kuwa na bima ya afya kwani sensa ya 2022 inaonyesha watoto chini ya Miaka 18 ni asilimia 31 ya Wananchi wote.


Licha hayo, Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa uzoefu wa Miaka saba wa kulihudumia kundi hilo la watoto kupitia utaratibu wa Toto afya kadi umewezesha Mfuko kufikia watoto 210,664 walio chini ya miaka18 Mfuko umepitia mambo mengi ya kujifunza ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi Ili kuboresha.
Ametaja changamoto hizo ni pamoja na usajili wa mtoto mmoja mmojw ambayo inachelewesha Utekelezaji wa dhana ya  bima ya afya ambayo inataka watu kujiunga kwa wingi.


Sanjari na hilo,Mfuko huo umeendelea kushirikiana na Shule zaSekondari na Msingi Ili kusajili wanafunzi na mwitikio unaonyesha hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea nayo Ili kuhakikisha watoto wengi zaidi wanasajiliww na kunufaika na bima ya afya.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »