Mkuu wa Mkoa wa shinyanga awaahidi wazee kuwaboreshea huduma za Afya

Mkuu wa Mkoa wa shinyanga awaahidi wazee kuwaboreshea huduma za Afya

Na Barnabas Kisengi Shinyanga MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amekutana na Wazee Manispaa ya Shinyanga kuzungumza nao, kufahamiana, huku akiwaahidi kuboresha huduma za Afya kwa wazee. Mkuu wa Mkoa amesema leo ni siku yake ya kwanza kuanza kazi mkoani humo, hivyo ameona kitu cha kwanza azungumze na wazee ili apate baraka pamoja na

Na Barnabas Kisengi Shinyanga


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amekutana na Wazee Manispaa ya Shinyanga kuzungumza nao, kufahamiana, huku akiwaahidi kuboresha huduma za Afya kwa wazee.

Mkuu wa Mkoa amesema leo ni siku yake ya kwanza kuanza kazi mkoani humo, hivyo ameona kitu cha kwanza azungumze na wazee ili apate baraka pamoja na kuchota busara zao ili auongoze Mkoa vyema na kuuletea Maendeleo.

“Leo ni siku yangu ya kwanza kufanya kazi mkoani Shinyanga kama Mkuu wa Mkoa, nimeona kitu cha kwanza kabisa nikutane na nyie wazee tufahamiane na kujitambulisha kwenu, naombeni sana ushirikiano wenu katika kuuongoza Mkoa huu kwa sababu wazee ni hazina ya Taifa,”amesema Mndeme.

“Nyinyi Wazee ndiyo mmeweka misingi imara ya uongozi, mmepigania uhuru wa taifa letu na kudumisha amani, hivyo sisi viongozi hatuna budi kuchota busara zenu, pamoja na kuwalea, kuwaheshimu, kuwalinda, na kuhakikisha mnapata huduma bora za matibabu kwa kutengewa madirisha ya wazee na upatikanaji wa madawa ya wazee na hakuna mzee kuandikiwa akanunue dawa,”amesema Mndeme.

Aidha, Mndeme amewaomba Wazee hao wasimamie Mmomonyoko wa maadili kwa vijana ambao kwa sasa wamekuwa wakikiuka mila na desturi za Kitanzania na kufanya vitendo vichafu vikiwamo vya Ubakaji na Ulawiti.

Katika hatua nyingine amekemea suala la mauaji ya wazee, na kutaka mauaji hayo licha ya kupungua bali yaishe kabisa,kwa sababu kuwa mzee siyo dhambi.

Naye Katibu wa Baraza la Wazee mkoani Shinyanga Anderson Lyimo, akisoma taarifa ya wazee kwenye kikao hicho, amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kukutana na wazee na kumuahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha na kuchochea maendeleo.

Katika Taarifa hiyo ametaja baadhi ya changamoto ambazo bado zinawakabili wazee na kuomba Serikali izishughulikie likiwamo suala la ukosefu wa madawa ya wazee kwenye baadhi ya vituo vya afya, wazee kutoshirikishwa kwenye vikao vya maamuzi hasa ngazi ya halmashauri, kutotengewa bajeti ya shughuli za wazee, kutekelezwa na watoto wao, pamoja na kutotungiwa sheria ya wazee.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »