SHINYANGA: WAMILIKI VIWANDA WAILALAMIKIA TANESCO UMEME KUKATIKA HOVYO

SHINYANGA: WAMILIKI VIWANDA WAILALAMIKIA TANESCO UMEME KUKATIKA HOVYO

BAADHI ya wamiliki wa Viwanda vya kukoboa na kusaga nafaka mkoani Shinyanga wamelalamikia kitendo cha kukatika kwa nishati ya umeme katika maeneo ya viwanda vyao hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha uzalishaji. Wamiliki hao wamedai changamoto ya kukatwa kwa umeme mara kwa mara inawaathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na kushindwa kuzalisha kwa

BAADHI ya wamiliki wa Viwanda vya kukoboa na kusaga nafaka mkoani Shinyanga wamelalamikia kitendo cha kukatika kwa nishati ya umeme katika maeneo ya viwanda vyao hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha uzalishaji.

Wamiliki hao wamedai changamoto ya kukatwa kwa umeme mara kwa mara inawaathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na kushindwa kuzalisha kwa wingi bidhaa na kujikuta wakipoteza wateja wao kutokana na wateja kukosa bidhaa wanazozihitaji.

Eliya Andrea ni miongoni mwa wananchi wanaofanya biashara ya ukoboaji wa mpunga na uuzaji wa mchele katika vinu vya kukoboa nafaka vilivyopo eneo la Ibinzamata manispaa ya Shinyanga amedai umeme kero ya kukatika umeme katika maeneo yao imezidi ambapo kwa wiki moja unaweza kukatwa siku nne au tatu.

Andrea amesema hali hiyo imekuwa ikiwasikitisha na kwamba iwapo isipopatiwa utatuzi wa haraka nchi ya Tanzania inaweza kujikuta ikipoteza wawekezaji kutoka nje ya nchi pamoja na wito wa mara kwa mara wa viongozi wakuu wa Serikali kuwataka wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza hapa nchini.

Neema Ezekiel mjasiriamali eneo la Ibinzamata na Dismas Mongela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kizumbi Food Trading Company wamesema kukatika mara kwa mara kwa umeme kunawaathiri kwa kiasi kikubwa na kwamba pamoja na hali hiyo bado wanalazimika kulipa mapato TRA kwa kiwango cha juu.

Wananchi hao wameiomba Serikali ifanye kila linalowezekana ili kuwezesha nishati hiyo muhimu ipatikane wakati wote na kwa uhakika ili waweze kuzalisha kwa wingi na kuiongezea Serikali mapato yake.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANESCO mkoani Shinyanga, Mhandisi Kulwa Mangara amekiri kuwepo kwa changamoto ya kukatika katika kwa umeme na kwamba hali hiyo inatokana na kupungua kwa kiwango cha uzalishaji katika gridi Taifa na si mkoa wa Shinyanga tu unaoathirika bali mikoa yote nchini inayopata umeme kutoka gridi ya Taifa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »