Wananchi wa Mkoa wa Kagera watakiwa kufuata Maelekezo ya wataalamu wa Afya Ili kuweza kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko

Wananchi wa Mkoa wa Kagera watakiwa kufuata Maelekezo ya wataalamu wa Afya Ili kuweza kuepuka magonjwa mbalimbali ya mlipuko

Na Mwandishi Wetu Kagera Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya amewaasa wananchi wa Mkoa wa Kagera kufuata maelekezo ya Wataalamu wa afya katika maeneo yao ili kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko.  Dkt. Mollel ametoa wito huo Machi 18, 2023 wakati akiongea na vyombo vya

Na Mwandishi Wetu Kagera


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya amewaasa wananchi wa Mkoa wa Kagera kufuata maelekezo ya Wataalamu wa afya katika maeneo yao ili kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko. 


Dkt. Mollel ametoa wito huo Machi 18, 2023 wakati akiongea na vyombo vya habari baada ya kufanya kikao na Wataalamu wa afya katika Mkoa huo ili kuona namna bora ya kupambana dhidi ya mlipuko wa magonjwa mbalimbali Mkoani Kagera.
“Tuendelee kuwaasa wananchi maelekezo yote ambayo Wataalamu wa afya wanayatoa mfano mambo ya kuzikana, hata kama mgonjwa hajaonesha dalili zinazofanana kama swala la maziko wayazingatie kwa Wataalamu na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya.” Amesisitiza Dkt Mollel


Naibu waziri wa Afya Dkt. Mollel ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa namna walivojitoa katika kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali tangu kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana Machi 16, 2023 Mkoani hapo.
Sambamba na hilo amewapongeza Watumishi wa afya katika ngazi zote, kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya zahanati kwa namna bora wanavoendelea kupambana katika utoaji huduma jambo ndio maana bali ya afya inaendelea kuimarika.


Dkt Mollel amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa pesa, vifaa, dawa na rasilimali watu ili kuhakikisha hali ya afya katika Mkoa wa Kagera inaimarika na utoaji huduma unakuwa bora.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »