KINANA AWAFUNDA VIONGOZI WA UWT

KINANA AWAFUNDA VIONGOZI WA UWT

Na Barnabas kisengi Dodoma Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa chama hicho kusema mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika maeneo yao.Kinana amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mfunzo ya siku mbili ya viongozi wa Umoja wa

Na Barnabas kisengi Dodoma


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa chama hicho kusema mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika maeneo yao.
Kinana amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mfunzo ya siku mbili ya viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya.
“Katika maeneo yenu hakikisheni mnakisemea chama na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia,na wala msione haya kusema ili wananchi wajue na hata katika chaguzi zijazo tusipate shida”amesema kinana
Aidha Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa amesema Chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia katika kipindi cha miaka miwili kila kata kuna alama ya maendeleo ameweka ikiwemo shule,zahanati,barabara na maendeleo ya watu hivyo tuna kila sababu ya kujisifia na kuusifia uongozi wa Mwenyekiti wa chama hiki.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Comredi kinana amesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufia lengo la kujenga jamii ya usawa.


Aidha Comredi kinana amesema mwakani kuna uchaguzi wa viongozi wa serikai za mitaa, ni vyema wanawake wakajitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na CCM itawapa ushirikiano wa kutosha.
“Kuelekea uchaguzi ujao jiandaeni na kuwahimiza wanawake kuwania nafasi zote za uongozi na ninawahakikishia kuwa CCM itawaunga mkono kwa hali na mali ili kuwa na wanawake wengi waliochaguliwa katika majimbo,”amesisitiza Comredi kinana


Katika hatua nyingine Comredi Kinana amewataka UWT kuhakikisha maamuzi mengi yanafanyika kupitia vikao na sio maamuzi ya mtu mmoja au kikundi cha watu bali yawe maamuzi ya vikao.


“Niwasihi tumieni vikao kuamua mambo sio makundi ya watu kila kitu lazima kijadiliwe kwa kina na kipite kwa hoja kwasababu ndani ya CCM hakuna maamuzi ya mtu mmoja au amri, na ninyi katika maeneo yenu hakikisheni ndani ya vikao huko ndio haki ya mtu itapatikana,”amesisitiza Comredi kinana


Kinana aliwataka viongozi hao kuto wahamisha hovyo viongozi kwani amebaini wengine wanashtukizwa bila kupewa taarifa ya uhamisho.
“Wenyeviti mpunguze kuhamisha watu hovyo kama mtu amekosea aitwe aelezwe kosa sio kuchukua maamuzi ya haraka una mualibia mtu mwelekeo, tujenge utamaduni wa kuambiana ukweli na msiogopane mtu anapokosea ,”amesema Comredi kinana


Makamu huyo aliwashauri viongozi hao kusoma vitabu mbaimbali vya chama ikiweo Ilani ya uchaguzi,sera,kanuni katiba vitawasaidia katika masuala mbalimbali ya uongozi.
“Someni katiba, kanuni, ilani, na sera vitawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za chama na kuongoza kwa kuzingatia misingi ya haki,”amesisitiza Comredi kinana.


Awali Mwenyekiti wa UWT Taifa Marry Chatanda amesema wanawake wanaridhika na kazi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia na ilani ya CCM inatekelezwa kwa kishindo.


Amesema katika kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita hakuna kilichosimama ndio maana waliandaa hafla ya kumpongeza Rais Dk.Samia kwa kazi nzuri alizozifanya.
“Sisi wanawake wa CCM hakika tumeridhishwa na uongozi wa Rais Dk.Samia na tunaahidi katika uchaguzi wa mwaka 2025 tutatoa fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu mwanamke mwenzetu,”amesema chatanda


Naye Katibu wa UWT Taifa Dk.Philis Nyimbi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuleta ustawi na kuwapatia viongozi maarifa namna ya kuongoza jumuiya hiyo katika ngazi zote na yamewashirikiaha viongozi 478 na wanatarajia Mafunzo hayo wanayoyapata wakilaliza watakwenda kutoa elimu hiyo katika ngazi ya kata na Mashina 
“Mafunzo haya ni mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wetu ukizingatia tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi mkuu mwaka 2025, hivyo kutokana na mafunzo haya watatakiwa kuyapeleka katika ngazi ya kata na matawi na kutuletea taarifa,”alisisitiza nyambi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »