Serikali kushirikiana na Wadau mbalimbali kukabiliana na kifua kikuu

Serikali kushirikiana na Wadau mbalimbali kukabiliana na kifua kikuu

Na Mwandishi wetu- Dodoma. Serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau katika sekta zote ili kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ifikapo mwaka 2030. Katibu  Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema hayo Katika kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara kilichofanyika katika ofisi za Waziri Mkuu Jijini Dodoma. “Ili

Na Mwandishi wetu- Dodoma.

Serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau katika sekta zote ili kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ifikapo mwaka 2030.


Katibu  Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema hayo Katika kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara kilichofanyika katika ofisi za Waziri Mkuu Jijini Dodoma. 
“Ili kudhibiti ugonjwa huu wa Kifua Kikuu ni muhimu kushirikiana na wadau wengi kama sekta ya afya, wadau sekta ya elimu, sekta ya usafirishaji na sekta nyingine mbalimbali.” amesema Dkt. Yonazi.


Kwa upande wake Mtaalamu Mshauri kutoka Stop TB Partnership (STP) Bw. Oscar Mukasa wakati akiwasilisha taarifa ya mpango kazi wa kudhibiti Kifua Kikuu amesema watu wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo  ni pamoja na watu wanaoishi katika  makazi duni, Watoto, Wavuvi na  wanafunzi wanaoishi bweni.


Kuna makundi mengine  ambayo yako hatarini kupata maambukizi Watu wenye VVU, watu wenye Utapiamlo, wachimbaji madini, wanaoishi na mgonjwa wa Kifua Kikuu, watoa huduma za afya na wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano.


Bw. Mukasa amewashauri wanaoishi katika mazingira hayo kuchukua tahadhari  za kujikinga na ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »