WAZIRI SIMBACHAWENE AZINDUA MPANGO SHIRIKISHI WA TAIFA WA KUZUIA NA KUKABILIANA NA UGONJWA WA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU KWA MWAKA 2023 – 2027

WAZIRI SIMBACHAWENE AZINDUA MPANGO SHIRIKISHI WA TAIFA WA KUZUIA NA KUKABILIANA NA UGONJWA WA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU KWA MWAKA 2023 – 2027

Na Moreen Rojas Dodoma. Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na uratibu  George Simbachawene amezindua mpango shirikishi wa taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu kuanzia mwaka 2023_2027. Waziri Simbachawene amehimiza Wizara ya afya kuhakikisha inafanyia kazi tetesi za ugonjwa na wagonjwa kufuatilia haraka ili kukabiliana na ugonjwa huo haswa maeneo yenye kupata

Na Moreen Rojas Dodoma.


Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na uratibu  George Simbachawene amezindua mpango shirikishi wa taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu kuanzia mwaka 2023_2027.


Waziri Simbachawene amehimiza Wizara ya afya kuhakikisha inafanyia kazi tetesi za ugonjwa na wagonjwa kufuatilia haraka ili kukabiliana na ugonjwa huo haswa maeneo yenye kupata milipuko ya mara kwa mara ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo.
“Kama tulivyoshirikina kuanzisha mpango huu niwaombe wadau wote kuhakikisha tunashirikiana na tunatekeleza kwa vitendo Maelekezo yote tulivyokubaliana”Alisisitiza Simbachawene
Simbachawene amezisihi ofisi za serikali za mitaa na tawala za mikoa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kunawa mikono na maji tiririka wakati wa kutoka msalani na kabla ya kuandaa chakula pamoja na kutumia maji safi na kuacha kula vyakula vichafu.
“Mpango huu unatoa muongozo muhimu utakao hakikisha sekta na taasisi zote zitatekeleza mpango huu ili kuepukana na ugonjwa huu wa hatari”Amesema Simbachawene.


Aidha waziri Simbachawene amesema kuwa mpango huu umeandaliwa kufuatia tathimini ya ugonjwa kwa maeneo yanayojirudia kupata ugonjwa huo ikiwemo sababu ni ukosefu wa maji safi na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na ugonjwa huu.


Simbachawene amesema kuwa Suala la kuzuia na kukabulina na ugonjwa wa kipindupindu ni sekta mtambuka ndio maana tumekusanyika kwani tatizo hili ni kubwa kukabiliana kwa pamoja.


Naibu Waziri wa afya Dkt.Godwin Molel ambaye amemwakilisha Waziri wa afya Ummy Mwalimu amsema kuwa wizara ya afya inajivunia Rais wetu Dkt.Samia Suluh Hassan kwa kuhakikisha wadau wanakwenda vizuri na kufanya kazi vizuri kwa kushirikiana na sekta ya afya kutoka visa 2022 hadi sasa kufikia 537.
“Kwa mwaka huu kwenye hospitali za taifa na kanda Rais ametoa shilingi bilioni 54 kwenye hospitali za  mikoa bilioni 54.4 na kwenye vifaa tiba shilingi bilioni 108″amesema Dkt Molel


Kwa Upande Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema wanamshukuru na kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluh Hassan kwa kuboresha miundombinu kwenye sekta ya afya ikiwemo vifaa tiba na kuboresha afya ya watu wake lakini hayo yote hayawezi kutimia kama hakuna mpango wa kuthibiti ugonjwa wa kipindupindu.
“Kama mkoa tutafuata taratibu zote mtakazotuambia ili kuhakikisha tunadhibiti magonjwa ya mlipuko hadi 2030 na kutokomeza kabisa ugonjwa wa kipindupindu na kuwa mfano kama makao makuu ya nchi”Amesema Shekimweri


Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la serve the children ambaye ni Mkurugenzi mtendaji Angela Kauleni amesema wanaishukuru serikali kwa kutoa ushirikiano katika mikoa ya katavi na manyara na wameweza kushirikiana vizuri na serikali za mikoa na wanashukuru hakuna magonjwa mapya.
” Tunafanya miradi ya maendeleo pamoja na miradi ya kujenga taifa kusaidia watoto kufikia malengo yao kuhakikisha kwamba watoto wanaishi na wanasaidiwa kujifunza kulindwa na kuhakikisha mtoto hafanyiwi ukatili wa aina yeyote”Amesema Angela


Aidha shirika hilo kwa kushirikiana na mganga mkuu wa serikali katavi na manyara waliweza kuendesha mafunzo ya mawasiliano,umuhimu wa kujenga choo,kuhusu ugonjwa na athari zake.
“Elimu juu ya usafi wa mazingira umekuwa ni hafifu lakini ahadi yetu ni kuendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha tunatokomeza kipindupindu katika nchi yetu ya Tanzania”Amesisitiz Angela.


Naye mwakilishi kutoka UNICEF Tanzania Bi.Maniza Zaman ameipongeza serikali kwa kuweza kushiriki vizuri kuhakikisha inapambana na ugonjwa wa kipindupindu, elimu itaokoa maisha kwani kila mtu ataelewa ni namna gani atajikinga dhidi ya kipindupindu na wala sio kutumia pesa kwani pesa si chochote muhimu ni usafi.
“Kuzindua mpango ni rahisi lakini utekelezaji wa mpango ndio muhimu zaidi lazima kuhakikisha tunatekeleza na kutoa elimu kwa wananchi kwa kushirikiana na waganga wa eneo husika”Amesema Bi Maniza


Mwakilishi kutoka World health organization(WHO) Tanzania amesema tumezindua kitu muhimu kwenye maisha,kuokoa maisha ya watu,hatutaki na tunataka kuhakikisha tunatokomeza kabisa kipindupindu Tanzania 2030.
” Kukusanya sekta zote kwa pamoja itafanya sekta ya afya kufanya kazi kwa urahisi ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu”


Uzinduzi wa mpango shirikishi wa taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu 2023_2027 umebebe kauli mbiu isemayo ushirikiano wa kisekta ni mkakati sahihi wa kuzuia,kukabiliana na kutokomeza kipindupindu nchini ifikapo 2030.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »