Serikali inaunga mkono jitihada za sekta binafsi za kukuza maendeleo.

Serikali inaunga mkono jitihada za sekta binafsi za kukuza maendeleo.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na sekta binafsi katika kuwaunganisha na kuwaletea maendeleo wazanzibari.Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Sera,Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe Hamza Hassan Juma kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na sekta binafsi katika kuwaunganisha na kuwaletea maendeleo wazanzibari.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Sera,Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe Hamza Hassan Juma kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya  Iftar iliyoandaliwa na benk ya NMB Tawi la Zanzibar iliyofanyika Kwenye ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.
Amesema Serikali inaunga mkono juhudi zinazochukuliwa na benk ya NMB za kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwaletea maendeleo mbali mbali wananchi pamoja na kupambana na umasikini.
Alhajj Hemed ameupongeza uongozi wa NMB kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuunga mkono jitihada za kimaendeleo  zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt Hussein Ali Mwinyi  katika kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wake.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameyataka mabenk mengine kuweza kushirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar na watanzania kwa ujumla.
Amesema  uamuzi unaofanywa na benk hio  wa kuwakutanisha wananchi katika Iftar ni ibada jambo ambalo linawaweka pamoja viongozi na wateja hasa katika kitpindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhan
Kwa upande wake Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Ndani wa Benk ya NMB Ndugu .BENEDICT BARAGOMWA amesema wameandaa IFTAR hio kwa lengo la kuwaweka karibu wateja, wananchi  na viongozi ikiwa ni miongoni mwa kuadhimisha miaka ishirini na tano (25) tokea kuasisiwa kwa benk hio.
Aidha Ndg BARAGOMWA amewataka waumini wa Dini ya kiislamu kuendelea kudumisha ibada,upendo na mshikamano wa dhati  na kuimarisha Imani  pamoja na kujiweka karibu na mwenyezimungu ili kupata fadhila za mwezi mtukufu wa ramadhan.
 Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)06 Aprili, 2023

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »