DINI INA MCHANGO MKUBWA WA KUJENGA MAADILI KWENYE TAIFA.

DINI INA MCHANGO MKUBWA WA KUJENGA MAADILI KWENYE TAIFA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua msikiti wa ‘Masjid Ali Bin Saif’ kabla ya kuuzindua, msikiti ambao umejengwa na familia ya Sheikh Seif Ali Seif, maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam Aprili 14, 2023. Sheikh Nassor na Sheikh Seif wamejenga msikiti huo wenye hadhi kubwa kwa niaba ya Baba yao ambaye ameshatangulia mbele ya haki. – Advertisement – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua msikiti wa ‘Masjid Ali Bin Saif’ kabla ya kuuzindua, msikiti ambao umejengwa na familia ya Sheikh Seif Ali Seif, maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam Aprili 14, 2023. Sheikh Nassor na Sheikh Seif wamejenga msikiti huo wenye hadhi kubwa kwa niaba ya Baba yao ambaye ameshatangulia mbele ya haki.

– Advertisement –

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya  kuzindua msikiti wa ‘Masjid Ali Bin Saif’ uliojengwa na familia ya Sheikh Seif Ali Seif, Vingunguti jijini Dar es Salaam Aprili 14, 2023. Sheikh Nassor na Sheikh Seif wamejenga msikiti huo wenye hadhi kubwa kwa niaba ya Baba yao ambaye ameshatangulia mbele ya haki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini waendelee kupiga vita vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa jamii ili kulifanya Taifa kuwa mahali salama kwa watoto na Watanzania kwa ujumla.

Ametoa wito huo leo Ijumaa (Aprili, 14, 2023) alipofungua msikiti wa ‘Masjid Ali Bin Saif’ uliopo Vingnguti jijini Dar es Salaam. Msikiti huo umejengwa na familia ya Sheikh Seif Ali Seif.

Amesema kuwa moja kati ya msisitizo mkubwa wa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto, mmomonyoko wa maadili

“Tukiachia mmomonyoko wa maadili, tunaweza kutengeneza Taifa ambalo halitakuwa na manufaa mbeleni, Viongozi wa dini mmekuwa mstari wa mbele katika kukemea ukatili dhidi ya watoto.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ni budi kwa Watanzania kuhakikisha wanapiga vita matendo yote yanayoharibu utamaduni, mila na desturi ya mtanzania “Tunayoyasikia huko duniani tuombe yasije hapa nchini na kama yapo tuyapige vita, Taifa hili leo tupo hapa na viongozi walioongoza nchi hii walisimamia kwenye mapambano dhidi ya mmomonyoko wa maadili”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka waumini wa dini ya kiislam kuutumia mwezi mtukufu wa ramadhan kuliombea taifa ili mwenyezi Mungu aendelee kuilinda na kudumisha amani, kuikinga dhidi ya maradhi na majanga mengine.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema amesema amevutiwa na ubora na uzuri wa msikiti huo. “Msikiti wa Ali bin Saif umejengwa kwa viwango vya juu sana hadi natamani na mimi pia ningekuwa mkazi wa Vingunguti ili na mimi nipate raha ya kusali kwenye Msikiti huu”

Naye Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omar ameipongeza familia ya Sheikh Seif Ali Seif kwa kujenga msikiti huo kwani ni sehemu bora kuliko sehemu zote duniani

Akizungumzia kuhusu msikiti huo wenye hadhi kubwa ambao umejengwa kwa niaba ya Baba yao ambaye ameshatangulia mbele ya haki. Sheikh Seif Ali Seif amesema msikiti huo unauwezo wa kuhudumia wanaume 600 na wanawake 150, ina vyumba vya madrasa 3

Pia katika ufunguzi huo ilifanyika ibada maalumu ya Kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wote wanaomsaidia majukumu yake.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »