RAIS MWINYI AHIMIZA WENYE UWEZO KUTOA SADAKA YA FUTARI KWA WENYE UHITAJI

RAIS MWINYI AHIMIZA  WENYE UWEZO KUTOA  SADAKA YA FUTARI KWA WENYE UHITAJI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk.Hussein Ali Mwinyi ameitaka jamii kwa kila mwenye uwezo kuendeleakuwasaidia wenye uhitaji ili kupata fadhila za mwezi huu mtukufu waRamadhani. Al- hajj Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi waliokwenye makundi maalumu wakiwemo wazee, wajane, watoto yatima na wenyeulemavu huko viwanja wa Mapinduzi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk.
Hussein Ali Mwinyi ameitaka jamii kwa kila mwenye uwezo kuendelea
kuwasaidia wenye uhitaji ili kupata fadhila za mwezi huu mtukufu wa
Ramadhani.


Al- hajj Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi walio
kwenye makundi maalumu wakiwemo wazee, wajane, watoto yatima na wenye
ulemavu huko viwanja wa Mapinduzi Square, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni mwezi wa neema na inampendeza
Mola, watu wote kuishi kwa upendo, ushirikiano na kusaidiana hasa kwa jamii
zenye uhitaji zisaidiwe kwa kadri ya uwezo watu waliojaaliwa nao.


Alisema msaada wa vyakula uliotolewa na taasisi ya Maendeleo ya “Zanzibar
International Development Organization” umekuja wakati jamii unauhitaji, hivyo,
Rais Dk. Mwinyi aliendelea kutoa wito kwa wadau wengine na wananchi wenye
uwezo kuendeleza moyo wa kuwasaidia wengine wenye uhitaji ili kujenga jamii
yenye kumpendezesha Mwenyezi Mungu.


“Chakula hiki kuwapa watu wasiokua na uwezo, Mwenyezi Mungu awalipe pepo
ndegu zetu wafadhili hawa” Dk. Mwinyi aliwaombea Kheri wafadhili waliotoa
msaada huo wa vyakula kwa makundi maalum.
Aidha, Rais Mwinyi, aliishukuru taasisi ya maendeleo ya “Zanzibar International
Development Organization” ambao walijitolea kutoa msaada huo wa vyakula na
mahitaji mengine kwa jamii hio.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, mmoja wa wanufaika wa sadaka hiyo, Jamila
Boraafya (Mwenye ulemavu wa kuona) alimshururu Rais Dk. Mwinyi kwa jitihada
anayoichukua kuwafikia wananchi wake wa makundi yote.
Alisema uongozi wake umekua mfano wa kuigwa wa viongozi wengine wa ngazi
zote katika kuwahudumia wanaowangoza.


“Tunakushukuru sana Mhe. Rais Dk. Mwinyi, juhudi zako tunaziona na upendo
wako kwetu wananchi wako, hakika wewe ni kiongozi wa mfano na Mwenyezi
Mungu ataendelea kukulipa mema kwa kututumikia, unafika hadi mataifa ya nje
kwaajili ya kutuhangaikia sisi wananchi wako, ahsate sana na Mola azidi kukulipa
kheri” alishukuru Jamila.

Zoezi kama hilo la ugawaji wa sadaka ya iftari kwa mwezi huu mtukufu
Ramadhan, Rais Dk. Mwinyi pia alilifanya kwa Wilaya nne za Pemba kwa mikoa
yote ya Kusini na Kaskazini wakati wa ziara yake ya siku mbili kisiwani himo,
iliyomalizika hivi karibuni.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »