WAZIRI MKUU:SERIKALI IMESAJILI MIRADI YA UWEKEZAJI 537.

WAZIRI MKUU:SERIKALI IMESAJILI MIRADI YA UWEKEZAJI 537.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021 hadi Januari, 2023 Serikali ilisajili jumla ya miradi ya uwekezaji 537 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 7,222. Amesema hayo leo Alhamisi (Aprili 20, 2023) alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki, kinachojengwa na Kampuni

Maelezo ya picha hayapo.
Inaweza kuwa picha ya Watu 5

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021 hadi Januari, 2023 Serikali ilisajili jumla ya miradi ya uwekezaji 537 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 7,222.

Amesema hayo leo Alhamisi (Aprili 20, 2023) alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki, kinachojengwa na Kampuni ya East Africa Commercial and Logistics Center kwenye eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, hatua hiyo imetokana na kuboreshwa kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kuimarisha Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja ili kuvutia wawekezaji kwa kupunguza kero na kurahisisha utoaji huduma.

Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa ongezeko la usajili wa miradi hiyo unatarajia kutoa ajira takriban 92,770 “Kiwango hiki ni kikubwa kuwahi kuandikishwa katika kipindi chochote tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961.

”Amesema kuwa, Serikali kupitia Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) imefanikiwa kusajili Miradi 38 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 139.70 na mauzo nje yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 191.04.

“Miradi hiyo ni mahsusi katika sekta zinazozalisha bidhaa zitokanazo na Kilimo, bidhaa za viwandani, bidhaa za Mifugo, bidhaa za Kemikali, bidhaa za madini na bidhaa za misitu”Mradi huo utakuwa na maduka 2060 yenye ukubwa wa jumla ya mita za mraba 75000 ambapo eneo hilo litakuwa na huduma zote za kibiashara ikiwemo mabenki na huduma ufungishaji na usafirishaji.

Pia, Mapato ya jumla kwa mwaka yatafikia zaidi ya USD Milioni 500 mradi huo ukiwa umekamilika hivyo kusaidia katika ukuaji wa pato la Taifa la Tanzania na kuongeza mapato ya kikodi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »