Waandishi wa Habari mtembue hakuna uhuru usio na mipaka.Rais Dkt.Mwinyi.

Waandishi wa Habari mtembue hakuna uhuru usio na mipaka.Rais Dkt.Mwinyi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein AliMwinyi ametoa wito kwa tasnia ya habari kuitumia fursa ya maadhimisho yasiku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kuweka mkazo kwenye uhuruwa kujieleza ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binaadamu, kwa kuangaziauhusiano baina ya uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa

Inaweza kuwa picha ya Watu 8 na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 6, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 3, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 3, jukwaa na maandishi yanayosema '0 vya Habari a Haki'
Inaweza kuwa picha ya Watu 3, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 8, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 3, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya umati
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 9, jukwaa na maandishi yanayosema 'UNITED NATIONS TANZANIA AMWA FRIEDRICH STIFTUNG Akademie BANK I•I KFW u ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani uuinda Mustakahali wa Haki kn'
Inaweza kuwa picha ya Watu 14, jukwaa na maandishi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali
Mwinyi ametoa wito kwa tasnia ya habari kuitumia fursa ya maadhimisho ya
siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kuweka mkazo kwenye uhuru
wa kujieleza ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binaadamu, kwa kuangazia
uhusiano baina ya uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na haki
nyengine.
Aidha, aliwaasa waandishi wa habari kushirikisha wahusika wote kwa madhumuni
ya kulinda uhuru wa vyombo hivyo, kuimarisha uhuru wa kujieleza, na kuweka
mazingatio ya haki za binaadamu kama kitovu cha kufanya maamuzi kwa ngazi za
kimataifa, kikanda na kitaifa.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa
vyombo vya habari duniani huko ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Kiembe
Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katika maadhimisho hayo, Rais Dk. Mwinyi pia aliwataka waandishi wa Habari
kutimiza ahadi zilizotolewa na kila nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ili
kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Pia Dk. Mwinyi aliwataka wadau wa vyombo vya habari kuitumia siku hiyo
kuisherehekea kwa kuungana na mashirika yanayotangaza masuala ya mazingira,
haki za wanawake, watoto, haki za kiasili, haki za kidijitali, vita dhidi ya ufisadi na
mengineyo.
Alisema, maadhimisho hayo ni jukwaa muhimu katika kuibua changamoto za
kisera na kuangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya kuendesha vyombo
vya habari nchini.
Akizungumzia sheria ya Habari, Rais Dk. Mwinyi alisema, Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar tayari imeandaa mswada wa sheria hiyo yenye madhumuni ya kufuta
Sheria iliyopo ya Usajili wa Magazeti, Wakala wa Habari na vitabu Sheiria nambari
5 ya mwaka 1988 ambapo marekebisho yake ni sheria nambari 8 ya mwaka 1997
na kutunga Sheria mpya ya Huduma za Habari na Mambo yanayohusiana na
hayo.
Dk. Mwinyi alieleza kwamba Mswada huo tayari uko Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
na unatarajiwa kutoa sheria nzuri itakayohusiana na masuala ya habari.
Alisema Zanzibar, imekuwa na kasi ya usajili mpya wa vyombo vya habari hasa
vya kielektroniki kupitia Tume ya Utangazaji baina yam waka 2020 hadi 2023. Kwa
mijibu wa tume hiyo Dk. Mwinyi alieleza jumla ya TV 21 za kawaida na 38 za
mitandaoni zimesajiliwa, jumla ya redio 27 zikiwemo za masafa ya FM na za jamii
zimesajiliwa.
Aidha, alizungummzia Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, magazeti na majarida
71 yamesajiliwa tangu mwaka 1998 hadi 2023. Shirika la Utangazaji Zanzibar
(ZBC) na Shirika la Magazeti ya Serikali ni vyombo vya habari vya Serikali
ambavyo navyo vimekuwa vikifanya kazi kubwa za kutoa taarifa kwa umma.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Mhandisi Andrew Kundo, aliviasa vyombo vya Habari nchini

kufanyakazi kwa kuzingatia, miongozo, kanuni na sheria zilipo katika utekelezaji
wa majukumu yao.
Naye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita,
alisema Serikali kupitia Wizara ya Habari itaendelea kushirikiana na wadau wa
vyombo vya habari nchini ili kuendelea kuwapasha habari wananchi.
Mkurugenzi kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania,
TAMWA, Joyce Shebe, aliomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuharakisha
mchakato wa Sheria ya Habari
Jumla ya magazeti 312 yalisajiliwa nchini hadi tarehe 20 Februari, mwaka huu,
ambapo baada ya Uhuru wa Tanganyika, kulikuwa na magezeti 10 tu.
Kwamujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi mwezi Februari
mwaka huu, jumla ya redio 218, televisheni 68, redio za mtandao nane, televisheni
za mtandao 391, blog, majukwaa 73 na cable operators 53 zimesajiliwa Tanzania
bara, ambapo taarifa za baada ya uhuru zinaonyesha tulikuwa na kituo kimoja tu
cha redio cha Tanganyika na hakukuwa na kituo cha televisheni hata kimoja,
blogs wala majukwaa ya mtandaoni.

IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »