ALHAJ DK.MWINYI ASHIRIKI SWALA YA IJUMAA MASJID TAUWHID FUONI

ALHAJ DK.MWINYI ASHIRIKI SWALA YA IJUMAA MASJID TAUWHID FUONI

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itajitahidi kutoa msaada kwa kadri itakavyowezekana kwa taasisi zilizobeba dhima ya kuwasafirisha mahujaji kwaajili ya ibada ya Hijja, kupitia taasisi ya Wakhfu na Mali ya amana ili kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa ibada ya hiyo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itajitahidi kutoa msaada kwa kadri itakavyowezekana kwa taasisi zilizobeba dhima ya kuwasafirisha mahujaji kwaajili ya ibada ya Hijja, kupitia taasisi ya Wakhfu na Mali ya amana ili kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa ibada ya hiyo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislam wakati wa ibada ya sala ya Ijumaa kwenye msikiti wa masjid – Tauhid  uliopo Fuoni, Wilaya ya Mjagharibi B.

Al – hajj  Dk. Mwinyi alisema, mara kadhaa kumejitokeza changamoto nyinyi kwa mahojaji wengi wanaotekeleza ibada ya hijja, aliasa kwamba mara hii seriali haitarajii kupokea taarifa zenye changamoto zozote.

“Mara nyingi siku za nyuma tulipata changamoto kadhaa wakati wa hijja, baadhi ya taasisi zinazowasafirisha mahujaji mara kadhaa hukabiliwa na changamoto mbalimbali na mara zote Serikali imekua ikiingilia kati, ni matumaini yangu na matarajio yangu kwamba changamoto zilizopita ziwe funzo kwa tunakoelekea sasa, Serikali haitarajii kuona changamoto hizo kujirejea tena.” Aliasa Al hajj Dk. Mwinyi.

Aidha, Al Hajj Dk. Mwinyi aliwasihi waumini wa dini ya kiislamu kwa kila mwenye uwezo ni vyema akatekeleza ibada hiyo akiwa mwenye siha kamili ili kujiepusha na baadhi ya changamoto zinazoweza kuepukika.

Al hajj Rais Mwinyi alieleza uwezo sio lazima mtu kuwa na pesa nyingi au mali kubwa lakini hata mtu kuuza kitu chake cha thamani au kutoa sehemu ya mali anazozimiliki kwaajili ya kutekeleza mapema ibada ya hijjah.

“Hijja ni ibada pia ni nguzo kwenye uislamu na sote tunawajibu kwa kila mwenye uwezo aone wajibu wake wa kwenda kufanya hijja”. Alinasihi Al – hajj Dk. Mwinyi.

Aidha, aliiomba taasisi ya  Wakhfu na Mali ya amana kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana ili mahujaji wakahiji kwa amani na salama bila kukumbana tena na changamoto walizopitia wenzao waliowatangulia.

Akizungumza msikitini hapo, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, alieleza hijja ni ibada ya muda mfupi lakini ni nzito kiimani,  hivyo aliwaasa wenye uwezo hasa vijana kutekeleza ibada hiyo wakiwa na nguvu na kuutumia ujana wao kwenye masuala ya khairati.

Naye, khatibu wa ibada ya sala ya ijumaa kwenye msikiti huo wa masjid Tauhid ambae pia ni Imamu mkuu, Sheikh Ali Suweid alieleza, hijja ni ibada inayojenga umoja na mshikamano wa waislamu kote ulimwenguni kama ilivyoamrishwa na Allah (S.W) alivyowausia waumini wa Kiislam kupitia kitabu chake kitukufu cha Quran kuwataka waislamu wote washikamane na washirikiane wala wasihitilafiane na kufarakana.

“Hakuna nchi yoyote kwenye ulimwengu huu wasasa, isipokuwa wakati huu wako kwenye maandalizi ya kukusanya mahujaji kwaajili ya ibada takatifu ya hijja” Alieleza Imamu huyo.

Alisema, waumini wa kiisalam kote ulimwenguni wako kwenye maandalizi ya  kuelekea mji mtukufu wa Makka, alieleza wapo watakao tembea kwa miguu, au vipando tofauti walivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu kwaajili ya kutekeleza ibada tukufu ya hijjah.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »