kutoa taarifa mapema za dalili za ugonjwa wowote ni kuokoa Maisha.

Jamii imeaswa kuwa na desturi ya kutoa taarifa mapema pindi panapotokea dalili za ugonjwa wowote ili kuokoa Maisha . Wito huo umetolewa na  mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Elimu ya Afya kwa Umma Beauty Mwambebule baada ya kutembelea Kijiji cha Kige,kitongoji cha Kiala Wilayani Muleba Mkoani Kagera  kuifariji familia ya Sifa Hamada iliyokumbwa na msiba

Jamii imeaswa kuwa na desturi ya kutoa taarifa mapema pindi panapotokea dalili za ugonjwa wowote ili kuokoa Maisha .

Wito huo umetolewa na  mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Elimu ya Afya kwa Umma Beauty Mwambebule baada ya kutembelea Kijiji cha Kige,kitongoji cha Kiala Wilayani Muleba Mkoani Kagera  kuifariji familia ya Sifa Hamada iliyokumbwa na msiba baada ya kumpoteza mtoto wake mwenye umri wa miaka 22.

Beauty amesema  marehemu hakufariki kwa ugonjwa wa Marburg kama jamii ilivyokuwa ikizua taharuki  huku akisisitiza  jamii kuwa na desturi ya kutoa taarifa mapema pindi panapotokea dalili za ugonjwa wowote ikiwemo Malaria ili mgonjwa kuwahi sehemu ya kutolea huduma za afya ikiwemo Zahanati,Vituo vya afya na hospitalini kupimwa na kupata matibabu kwa haraka.

“Kwa hiyo bado tunatakiwa sisi kama jamii hata tunaambiwa mwenzetu aliyefariki haijasababishwa na ugonjwa wa Marburg  wito tuendelee kuchukua tahadhari kwenye familia zetu kuendelea kunawa  mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono  ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko,kwa hiyo pia kutoa taarifa mapema kwanza ni tiba kwa sababu unamuwahisha akaangaliwe na watalaam zaidi kuliko kukaa ndani, hivyo unaweza kumwokoa zaidi hata kama ni Malaria unamwokoa”amesema.

Naye Afisa Lishe Mkoa wa Kagera Joanitha Jovin amezungumzia umuhimu wa kula mboga za majani na matunda katika kuimarisha afya.

“Tunapokula mboga za majani ni muhimu kula na matunda kwa pamoja na mboga ya majani ukiipika isiive sana ujani ubaki kama inapokuwa shambani kwani mboga za majani na matunda zinaimarisha sana afya zetu”amesema.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Abdallah Mohammed ambaye ni kaka yake na Sifa Hamada pamoja na Aisha Hussein wametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa kuwa mstari wa mbele katika suala zima la  utoaji wa elimu na ufuatiliaji wa magonjwa kila maeneo ikiwemo vijijini na mjini.

“Naishukuru Serikali na mliofika hap ana kutupa majibu kamili kuhusu ugonjwa na kilichonifurahisha kwanza ni kuhusu huduma zilizotolewa na serikali tangu mgonjwa akiugua hadi kifo ,mzidi kutuangalia zaidi namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan”amesema Abdallah Mohammed”

Nimejifunza kunawa mikono mara kwa mara hata nikishika jani la mgomba ni muhimu kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni tunaona huduma zenu nashukuru tunazidi kujifunza “amesema Aisha Hussein.

Ikumbukwe kuwa  katika ziara hiyo ya kutembelea Wilayani Muleba watalaam mbalimbali wa Afya  wameambatana akiwemo  Beauty Mwambebule kutoka Wizara ya Afya, Elimu ya Afya kwa Umma, Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF) Stanley Magesa,Red Cross Society,wawakilishi kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa,pamoja na baadhi ya watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ambapo  pia  jumla ya watu 36 pamoja na watumishi 14 wamenufaika na elimu ya afya kwa ujumla.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »