Wakazi wa vijiji tisa wamepata elimu ya matumizi ya mfumo wa kushughulikia malalamiko.

Wakazi wa vijiji tisa vya kata ya Ihahi na Mapogoro Wilayani Mbarali mkoani Mbeyawamepatiwa elimu ya matumizi ya mfumo wa kushughulikia malalamiko wenyelengo la kurahisisha utekelezaji wa mradi wa kukuza na kuendeleza utalii kusinimwa Tanzania (REGROW) ili kuwa na uelewa wa pamoja katika hatua mbalimbaliza utekelezaji wa mradi huo. Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo

Wakazi wa vijiji tisa vya kata ya Ihahi na Mapogoro Wilayani Mbarali mkoani Mbeya
wamepatiwa elimu ya matumizi ya mfumo wa kushughulikia malalamiko wenye
lengo la kurahisisha utekelezaji wa mradi wa kukuza na kuendeleza utalii kusini
mwa Tanzania (REGROW) ili kuwa na uelewa wa pamoja katika hatua mbalimbali
za utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamezungumza na kueleza manufaa
waliyoyapata kutokana na mafunzo hayo ikiwemo hatua mbalimbali za kuwasilisha
malalamiko ambayo ni njia ya kuwasaidia kuondokana na migogoro ya aina tofauti.

wakizungumza katika semina hiyo watoa mada kutoka Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji NIRC Mhandisi Fumba Malima pamoja na Daudi Mangu, wamesema
mfumo wa kushughulikia malalamiko umelenga kutatua changamoto zinazoweza
kurudisha nyuma maendeleo ya mradi huo unaolenga kukuza utalii na kuinua pato la
wakulima kutokana na ujenzi wa miundombinu katika skimu za umwagiliaji hivyo
kuruhusu maji kurejea katika mito kwa matumizi ya wanyamapori.


Mhandisi Fumba Malima – Mwezeshaji Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC.Daudi Mangu – Mwezeshaji Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC.
Mradi wa Regrow umelenga kukuza utalii kusini mwa Tanzania kwa kuboresha
Miundombinu ya Umwagiliaji ikiwemo ujenzi wa mfumo wa utoroshaji maji katika
skimu za Umwagiliaji kurudi katika mto Ruaha Mkuu kwa matumizi ya wanyama

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »