TTB YASHIRIKI TAMASHA LA KUDUMISHA MILA NA TAMADUNI ZA KIAFRIKA.

TTB YASHIRIKI TAMASHA LA KUDUMISHA MILA NA TAMADUNI ZA KIAFRIKA.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki katika Tamasha la kudumisha na kuhifadhi Mila na Tamaduniza Kiafrica kwa ajili ya kizazi kijacho ambapo Bi Esta Solomoni , Mkuu wa ofisi ya TTB kanda yaKaskazini alipata nafasi ya kutoa wasilisho kuhusu utamaduni za kitanzania, vivutio vya utalii vyaTanzania pamoja na fursa za Uwekezaji zilizopo katika sekta ya


Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki katika Tamasha la kudumisha na kuhifadhi Mila na Tamaduni
za Kiafrica kwa ajili ya kizazi kijacho ambapo Bi Esta Solomoni , Mkuu wa ofisi ya TTB kanda ya
Kaskazini alipata nafasi ya kutoa wasilisho kuhusu utamaduni za kitanzania, vivutio vya utalii vya
Tanzania pamoja na fursa za Uwekezaji zilizopo katika sekta ya utalii.
Tamasha hili la siku tano (5) limefanyika katika Makumbusho ya Viumbe jijini Arusha kuanzia tarehe
22 – 27 Juni, 2023. Tamasha limeweza kuvutia washiriki kutoka nchi za Afrika Kusini, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Zambia, Zimbabwe, America, Ujerumani, Uingereza ,Costa Rica, Morocco, Nigeria,
Ghana, Senegal, Taiwan, Zanzibar, Congo DRC, Ufaransa, Uholanzi, Burkina Faso, Cote D’Ivoire, Benin
na Jamaica.
Aidha, Washiriki wameweza kushiriki zoezi la kupanda miti na kupata burudani za muziki na ngoma
za utamaduni wa Makabila ya Tanzania. Bodi ya Utalii Tanzania inaendelea na mkakati wake wa
kutangaza utalii kupitia matukio ya Kitaifa na kimataifa yanayofanyika nchini Tanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »