Mussa Mansoor amemkabidhi jezi na mipira yenye thamani ya shilingi milioni 25.

Mussa Mansoor amemkabidhi jezi na mipira yenye thamani ya shilingi milioni 25.

MDAU wa michezo Kibaha Mkoa wa Pwani Mussa Mansoor amemkabidhi Mkuu wa Mkoa Abubakar Kunenge jezi na mipira yenye thamani ya shilingi milioni 25 kwaajili ya michezo ya Wanafunzi wa shule za msingi UMITASHUMTA mkoa wa Pwani.Mansoor ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Pwani na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa

MDAU wa michezo Kibaha Mkoa wa Pwani Mussa Mansoor amemkabidhi Mkuu wa Mkoa Abubakar Kunenge jezi na mipira yenye thamani ya shilingi milioni 25 kwaajili ya michezo ya Wanafunzi wa shule za msingi UMITASHUMTA mkoa wa Pwani.
Mansoor ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Pwani na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa Pwani amemkabidhi Kunenga vifaa hivyo kwenye hafla ya kukabidhiwa zawadi kwa washindi wa michezo ya shule za msingi zinazotoka halmashauri 9 zinazounda Mkoa, huku akitoa wito kwa wadau wengine kusaidia kuinua vipaji mbalimbali.
“Nikiwa mdau wa michezo nimeguswa kudhamini michezo hii inayoibua vipaji vya vijana wetu kuanzia shule za msingi, rais wetu Samia Suluhu amekuwa mstari qa mbele kuhakikisha michezo inasonga mbele,” alisema Mdau huyo.
Katika kuthibitisha sekta ya michezo, sanaa na michezo ametolea mifani mbalimbali ikiwemo ya sanaa huku akimtaja Mwanamuziki Daimond Pratnum na wengine ambao kwa kutumia taaluma zao wanachangia pato la Taifa.
Kwa upande wake Kunenge alimpongeza Mansoor kwa kuguswa huko, huku akieleza kuwa Mkoa unathanini juhudi hizo zinazounga mkono kazi kubwa ya Rais katika kuendelea michezo.
“Kuna jambo umelizungumzia linalohusiana na viwanja vya michezo, Mkoa unaendelea na juhudi hizo pia tunamshukuru Rais Mstaaafu Dkt. Jakaya Kikwete pale Kijiji cha Msoga kuna uwanja wa kisasa unataraji kujengwa,” alisema Kunenge.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »