Rais Dkt.Mwinyi Amezungumza na Wazee wa BWELEO.

Rais Dkt.Mwinyi Amezungumza na Wazee wa BWELEO.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein AliMwinyi amesema Serikali inaposaini mikataba na wawakezaji mbalimbaliwanaowekeza nchini kipaumbele cha kwanza ni kuwanufaisha wananchiwazawa wa eneo linaloekezwa.Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipozungmza na viongozi na wazee wa Barazala Wazee wa Bweleo waliofika Ikulu, Zanzibar kumtembelea.Alisema, lengo la Serikali kuita wawekezaji ni kuongeza Utalii

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali
Mwinyi amesema Serikali inaposaini mikataba na wawakezaji mbalimbali
wanaowekeza nchini kipaumbele cha kwanza ni kuwanufaisha wananchi
wazawa wa eneo linaloekezwa.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipozungmza na viongozi na wazee wa Baraza
la Wazee wa Bweleo waliofika Ikulu, Zanzibar kumtembelea.
Alisema, lengo la Serikali kuita wawekezaji ni kuongeza Utalii ili kukuza uchumi wa
nchi na kuwanufaisha wananchi wake sio kuwaumiza.
“Serikali inapokubaliana na wawekezaji, kipaumbele cha kwanza anachoambiwa
mwekezaji ni kuwanufaisha wananchi wa eneo linaloekezwa, kama wananchi
wanashughuli zao za kiuchumi kwenye eneo hilo, basi aziboreshe sio kuziondosha
pia awafikishe huduma nyingine muhimu zaidi za jamii ikiwemo maji safi,
kuwajengea vituo vya afya, masoko, skuli au barabara” Alifahamisha Dk. Mwinyi.
Aidha, aliwataka wazee wa Kijiji cha Bweleo kushirikiana na viongozi wao wa
ngazi zote kukaa pamoja na kuzungumza na wawekezaji wa eneo hilo ili waeleze
matatizo yao kwaajili ya kuyapatia ufumbuzi.
Pia, aliwataka Wizara ya Kazi na Uwekezaji na Mamlaka ya Uwekezaji, Zanzibar
(ZIPA) kukaa pamoja na baraza la wazee wa Bweleo ili kusikiliza changamoto zao
zinazohusiana na uwekezaji kwa nia ya kuzipatia ufumbuzi.
Rais Dk. Mwinyi aliwahakikisha wazee hao ujenzi wa kiwanja kikubwa cha
michezo kama ambavyo mipango ya Serikali ilivyoahidi kujenga viwanja vya
michezo kwa wilaya zote za Unguja na Pemba pamoja na kuwaahidi ujenzi wa
barabara yao ya ndani ambayo kwasasa iko kwenye changamoto ya mashimo
baada ya kuathiriwa na mvua za hivi karibuni.
Wakizungumza kwenye kikao hicho, walimpongeza Rais kwa jitihada zake
anazoendelea kuwatumikia wananchi wa Zanzibar na kuongeza mwanya wa
waletea maendeleo makubwa hasa kwenye jitihada zake za kushajihisha utalii na
kuongeza wawekezaji wengi nchini jambo walilolieleza limewaongezea tija
wanacnchi mbali ya kupata ajira lakini funza nyingi za uchumi na biashara
zimeongezeka.
Aidha, walimshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa jitihada zake za kuikuza na kuiboresha
Bweleo kimaendeleo kwa kukuwa huduma za utalii, wawekezaji kuongezekana
kuimaisha miundombili ya Kijiji hicho.
Waliiomba Serikali linapokuja suala la uwekezaji wanavijiji waangaliwe kwa nafasi
ya upendeleo katika kuzikimbilia fursa ikiwemo ajira, kuwezeshwa na kupatiwa
misaada ya maendeleo pamoja uhusiano mzuri wa ushirikiano baina yao
wawekezaji.
Kijiji cha Bweleo kiko Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi,
Unguja
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »