Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itafanikishe miradi iliyoidhamiria kwa Maendeleo ya wananchi wake.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itafanikishe miradi iliyoidhamiria kwa Maendeleo ya wananchi wake.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inajitahidi kupambana maeneotofauti ili ifanikishe miradi yake iliyoidhamiria kuifanikisha kwaajili yakuendelea kuwaletea Maendeleo wananchi wake.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyiameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirikala Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Bi. Christine Musisialiefika kumtembelea.Dk. Mwinyi alisema

Inaweza kuwa picha ya Watu 2, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 6 na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya Watu 2, chumba cha habari na maandishi yanayosema 'RAIS'

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inajitahidi kupambana maeneo
tofauti ili ifanikishe miradi yake iliyoidhamiria kuifanikisha kwaajili ya
kuendelea kuwaletea Maendeleo wananchi wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi
ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Bi. Christine Musisi
aliefika kumtembelea.
Dk. Mwinyi alisema daima Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalishukuru Shirika
la Kimataifa la UNDP kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali kwenye masuala
mbalimbali ya maendeleo.
Alisema SMZ na UNDP wana ushirikiano mzuri na kulipongeza Shirika hilo kwa
kuendelea kuiunga Mkono Tanzania ikiwemo Zanzibar hasa kwa kuiongezea
nguvu za kifedha Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi utendaji kazi Serikalini, PDB,
Zanzibar.
“Tunahitaji kuiwezesha zaidi PDB ili kuhakikisha inafanikisha ipasavyo majukumu
yake” alieleza Rais Dk. Mwinyi.
Rais Dk. Mwinyi alimwelezea mgeni wake huyo ushirikiano anaoupata kwa PDB
katika kutekeleza majukumu yake, hivyo aliipongeza UNDP kwa kuiunganga
mkono.
Alisema Serikali imeweka nguvu zake huko bila ya kutegemea bajeti kutoka
Serikali kuu pekee badala yake inahangaika kwa wadau mbalimbali wa
maendeleo ili kuiongezea bajeti.
Aidha Rais Dk. Mwinyi aliridhia ombi la UNDP la kukutana pamoja kwa baadhi ya
Mabalozi ambao ni wadau wa maendeleo wa shirika hilo wakiwemo Canada,
Uingereza na Norway.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwakilishi huyo wa UNDP, Christine Mwasisi
alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa uongozi wake wa kuendeleza amani na
kuendelea kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
Alimueleza Rais Dk. Mwinyi UNDP kwasasa inatekeleza miradi sita barani Afrika
ikiwemo mitatu kwa Tanzania ambapo Zanzibar wanashirikiana na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza miradi ya kupambana na matukio ya
Uhalifu Zanzibar, ambapo alieleza mradi huo wanashirikiana na Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashitaka chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza na Umoja wa
Ulaya (EU).
Alieleza mradi mwengine ni uwezeshaji kwenye masuala ya utawala wa kisheria
ambapo alieleza mradi utaangalia haki na wajibu kwenye masuala ya jinsia
ikiwemo masuala ya wanawake na watoto ambapo alieleza mradi huo unatarajiwa
kushirikiana na Baraza wa Wawakilishi Zanzibar.
Pia Bi. Musisi alieleza mradi mwengine utahusisha masuala ya fedha ambao
Mwakilishi huyo alisema tayari timu ya mradi huo imeshakutana na Waziri wa

Fedha wa Zanzibar Dk. Saada Mkuya Salum na kujadiliana kwa hatua za awali na
wadau wa wizara hiyo.
Aidha, mbali na mambo mengine pia mgeni huyo alimueleza Rais Dk. Mwinyi
kwamba UNDP ilivyojipanga kufanyakazi na Sekta ya Uchumi wa Buluu pamoja
na sekta ya Mazingira endelevu.
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »