Shinyanga yaja na mkakati wa kuwanufaisha wakulima wa Choroko.

Shinyanga yaja na mkakati wa kuwanufaisha wakulima wa Choroko.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi, Zainab Telack ameagiza Maafisa Kilimo Mkoani Shinyanga kutoa elimu ya mfumo wa stakabadhi gharani kwa wakulima wa zao la choroko ili waache tabia ya kuuza mazao yakiwa bado kuepuka kuwanufaisha wanunuzi badala ya wakulima ambao wanatumia nguvu nyingi kuandaa mazao hayo. Mkuu wa Mkoa amesema hayo jana wakati wa


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi, Zainab Telack ameagiza Maafisa Kilimo Mkoani Shinyanga kutoa elimu ya mfumo wa stakabadhi gharani kwa wakulima wa zao la choroko ili waache tabia ya kuuza mazao yakiwa bado kuepuka kuwanufaisha wanunuzi badala ya wakulima ambao wanatumia nguvu nyingi kuandaa mazao hayo.

Mkuu wa Mkoa amesema hayo jana wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku moja kilichowakutanisha  wadau wa zao la choroko Mkoani Shinyanga ili kujadili namna bora ya matumizi ya mfumo wa stakabadhi gharani kwa lengo la kuhakikisha unaleta tija kwa wakulima wa zao hilo na taifa kwa ujumla.

Bi. Telack aliongeza kuwa kwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani itawezesha wanunuzi wa zao la choroko kujua sehemu sahihi ya kupata zao hili likiwa katika ubora na kuepuka kuibiwa fedha zao na matepeli.

Aidha Bi. Telack aliongeza kuwa ni agizo la serikali kuhakikisha mazao ya aina ya kunde yanatumia mfumo stakabadhi gharani kama ilivyo kwa zao la korosho na sasa Shinyanga kwa kuanzia inaanza na zao la Choroko na baadae itahamishia nguvu zake kwenye zao la dengu na mpunga lengo likiwa kuahakikisha wakulima wa mazao haya wanapata faida ya jasho lao na kujiletea maendeleo.

‘’Nataka kuona wakulima Mkoani Shinyanga wakiwa na uwezo wa kusomesha watoto, kujenganyumba bora na kufaidika na jasho lao sio mkulima analima mpunga katika maji mengi lakini mnunuzi ananunua mpunga bado ukiwa shambani nakuvuna gunia sitini kwa kumlagai mkulima kwa kumpatia bodaboda.’’Amesema Bi. Zainab Telack 

Aidha Bi. Telack alimwagiza Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Simon kukutana na viongozi wa vyama vya msingi na Cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga(SHIRECU) kuweka mikakati ya pamoja ya kutoa elimu kwa wakulima ili wajue faida za kutumia mfumo wa stakabadhi gharani.

Naye Kaimu Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Simon alisema kuwa changamoto ya kushindwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani inapelekea kushindwa kuwa na takwimu sahihi za zao hilo, kuendelea kuwepo kwa utoaji vibali holela vilivyokuwa vikitolewa na Halmashauri bila kupitia vyama vya Msingi.

Bi. Hilda aliongeza kuwa vibali hivyo vilikuwa vikitolewa kwa wanunuzi wa kati ambao kimsingi ndio wapinzani wa mfumo wa stakabadhi gharani na hivyo kuendelea kumyonya mkulima kwa kununuoa choroko kwa bei za chini akitaja pia changamoto ya wakulima kukosa uvumilivu wa kusubili malipo kuwa ni sababu pia ya kushindwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa aliwaambia wadau wa kikao hicho kuwa viongozi wa vyama msingi mkoani humo ni tatizo sana kwakuwa hawajui uchungu wa wakulima kwani hawana hata shamba moja kazi yao imekuwa ni kuongea maneno maneno tu nakuwataka wakulima kuchagua viongozi ambao pia wana mashamba ya zao hilo.

Suala la Mfumo wa Stakabadhi Shambani sio jipya lakini kumekuwepo changamoto mbalimbali za utekelezaji wa mfumo huo ndio maana Mkoa unajipanga upya kuhakikisha unaondoa changamoto zilizopo na kutafuta namna bora ya uendeshaji mfumo huo kwa kushirikisha wadau wa zao hilo.

Na Barnabas kisengi .

SHINYANGAJanuary  12 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »