Mh.Kipanga ametoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa VETA nchini kuhakikisha ujenzi wa chuo cha veta Mafia unakamilika.

Mh.Kipanga ametoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa  VETA nchini kuhakikisha ujenzi wa chuo cha veta Mafia unakamilika.

NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga ametoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa  Chuo cha VETA nchini pankras Bujulu kuhakikisha ujenzi wa chuo cha veta wilayani Mafia kinakamilika kwa wakati. Kipanga ametoa matatizo hayo akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani mafia ambapo alitembelea na kukagua ujenzi wa chuo hicho pamoja na taasisi

NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga.


NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga ametoa miezi mitatu kwa Mkurugenzi wa  Chuo cha VETA nchini pankras Bujulu kuhakikisha ujenzi wa chuo cha veta wilayani Mafia kinakamilika kwa wakati.

Kipanga ametoa matatizo hayo akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani mafia ambapo alitembelea na kukagua ujenzi wa chuo hicho pamoja na taasisi zingine za elimu na kutoridhishwa na kazi ya ujenzi huo.

“Ujenzi huo ulitakiwa ukamilike tangu  Novemba mwaka jana lakini chakusikitisha hadi sasa bado haujakamilika hivyo nawapa miezi mitatu kuhakikisha mradi  unakamilika na  wanafunzi wanaaza kusoma”amesema kipanga

“Ndugu zangu hapa tatizo kubwa la kuchelewa kukamilika  kwa mradi ni kutokana na kazi hizi kuachiwa kwa mafundi ambao hawana uzoefu ,jambo ambalo linakwamisha mradi kushindwa kufikia mwisho.”amesema Kipanga

Mradi huu unagharimu  pesa za serikali ya awamu ya Tanzania Shilingi bilioni 1.6 ambapo hadi kufikia leo zimeshatumika Shilingi milioni 700 na mradi bado haujakamilika hivyo nimetoa miezi mitatu kuanzia leo hii kuhakikisha mradi huu unamalizika  na wanafunzi wanaanza kusoma.”amesema Kipanga

Katika hatua nyingine naibu waziri huyo alitoa maelekezo kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU  wilayani hapo kuhakikisha wanafuatilia matatizo aliyojitokeza kwenye miradi yote ambayo ameitembelea ili kubaini kama kuna  ubadhilifu wa fedha za miradi hiyo. 

Naibu waziri kipanga amesema lengo nikuona mradi hiyo inatekelezeka kwa wakati ili vijana wanaomaliza elimu ya msingi na hawajabahatika kuendelea wanapata fursa ya kwenda kusoma chuo cha veta lakini hata wale ambao wamemaliza kida to cha none na sita na wamekosa nafasi ya kwenda mbele na wanatamani kusoma ufundi na wenyewe waweze kupata nafasi ya kusoma chuo cha veta.

” Nawaagiza takukuru chunguzeni kwenye maeneo haya ambayo nimeyatolea maagizo lakini pia kuna maeneo ambayo nimetilia mashaka yachunguzeni na kimsingi tunakwenda kwenye Tanzania ya viwanda sasa kama hivyo lazima vyuo hivi vikamilike ili watoto wetu waweze kupata nafasi za kusoma

Kipanga amesema kuwa baada ya kukagua chuo na taasisi zingine atakwenda Tanesco ili kuhakikisha umeme unakuwepo  na watu wanafanya kazi usiku na mchana ili malengo ya ndoto za mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli Zitimie

Pia naibu waziri alikemea vikali kitendo cha mkandarasi mmoja kupewa kazi zaidi ya moja hali inayochelewesha kukamilika kwa wakati miradi hiyo ambapo aliwataka wafanyakazi hao kutokuondoka Mahala pa pakazi kwani miradi ya Serikali ni ya kimkakati kila kitu kinafanywa kwa malengo.

Naibu waziri kipanga aliipongeza  ofsi ya udhibiti ubora wa shule wilaya Mafia kwa kazi ambayo ambayo wamefanya kwani wameweza kusimamia  ujenzi wa jengo lao na fedha walizopewa na Serikali zimetumika vizuri hadi chenji  imebaki na wameonyesha uzalendo mkubwa. 

Na Barnabas kisengi.

Mafia.

January 12 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »