Mkuu wa shule ya secondary Mbulu asimamishwa kazi, afisa elimu atakiwa kujieleza.

Mkuu wa shule ya secondary Mbulu asimamishwa kazi, afisa elimu atakiwa kujieleza.

Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali ya mitaa (TAMISEMI)  Mh Devidi Silinde amemsimamisha kazi mkuu wa shule ya secondary wilayani mbulu huku akimwagiza afisa elimu secondary kuandika barua ya kujieleza kwanini wamemdangaja juu ya bei ya ununuzi wa saruji na kutokamilika kwa ujenzi wa shule wilayani mbulu. Silinde ametoa kauli hiyo

Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali ya mitaa (TAMISEMI)  Mh Devidi Silinde amemsimamisha kazi mkuu wa shule ya secondary wilayani mbulu huku akimwagiza afisa elimu secondary kuandika barua ya kujieleza kwanini wamemdangaja juu ya bei ya ununuzi wa saruji na kutokamilika kwa ujenzi wa shule wilayani mbulu.

Silinde ametoa kauli hiyo wilayani mbulu alipokuwa katika maendeleo wa ziara ya kikazi mkoani manyara kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na secondary  katika maeneo mbalimbali hapa nchini katika msimu huu wa mwaka 2021

“Hapa sasa mkuu wa shule hii nakusimamisha kazi kuanzia sasa na kuwaagiza takukuru wafanye uchunguzi wa majengo haya matatu hadi sasa hayajakamilika na mmetumia fedha ya serikali nyingi tena unanidanganya hapa saruji umenunua kwa bei ya mfuko moja kwa shilingi elfu 18 hii sijawahi kuona hapa Tanzania ndio naisikia hapa mbulu ni uwongo mtupu humu sasa takukuru fanyeni kazi yenu huyu mkuu wa shule namsimamisha kazi kwanza kwa kunidanganya kunisomea taarifa ya uwongo” amesema silinde

Pia swala la pili ni kwa afisa elimu secondary nahitaji uniandikie barua ya kujieleza kwanini mmenisomea taarifa ya uwongo pia kwanini umeshidwa kusimamia ujenzi huu wa vyumba vitatu vya madarasa havijakamilika hadi sasa wakati serikali ilishawaletea fedha zote za ujenzi huu wa vyumba vya madarasa

“Tena nakushanga hata wewe afisa elimu secondary unashirikiana na mkuu wako wa shule kunidanganya Mimi hebu kajitathimini kweli kama unatosha kuwa katika nafasi hiyo maana mimi naona nafasi hiyo inskushinda kabisa”amsema Silinde

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mbulu amemwahidi naibu waziri Tamisemi kuwa maelekezo yote aliyoyatoa katika ukaguzi wa miradi yote ya elimu ambayo imekutwa na dosari atahakikisha wanaifanyia kazi na kuikamilisha akishirikiana na wajumbe wa kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya yake kwa haraka ili wanafunzi wasipate shida katika msimu huu wa masomo. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »