Mamlaka ya mawasiliano ya Uganda imeyaamuru makampuni ya huduma za intaneti, kuifunga mitandao ya kijamii siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika. Katika barua ambayo shirika la habari la AFP limeipata, mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano ya Uganda UCC Bi. Irene Sewankambo ameyaagiza makampuni ya mawasiliano kusitisha mara moja matumizi ya mitandao ya kijamii na
Mamlaka ya mawasiliano ya Uganda imeyaamuru makampuni ya huduma za intaneti, kuifunga mitandao ya kijamii siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.
Katika barua ambayo shirika la habari la AFP limeipata, mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano ya Uganda UCC Bi. Irene Sewankambo ameyaagiza makampuni ya mawasiliano kusitisha mara moja matumizi ya mitandao ya kijamii na majukwaa ya kutuma ujumbe mtandaoni.
Uamuzi huo umetajwa wazi kuwa ni ulipaji kisasi wa hatua ya mtandao wa Facebook wa kufuta akaunti zinazounga mkono serikali zinazojaribu kudhibiti mjadala wa umma kuelekea uchaguzi mkuu.
Kampuni ya Facebook ilisema hapo jana kwamba akaunti hizo zinahusishwa na wizara ya habari na teknolojia.
Mitandao iliyowekwa katika orodha ya kufungiwa ni Facebook, Twitter, WhatsApp na Viber.
Baadhi ya mitandao tayari imeripotiwa kutopatikana kuanzia leo.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *