MTANDAO WA WIZI WA MADAWA WABAINIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI

MTANDAO WA WIZI WA MADAWA WABAINIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Kesi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) waliofukuzwa kwa kuwapa wagonjwa dozi kubwa za dawa kuliko mahitaji, wakitumia jina la daktari “hewa”, imeanika mbinu za wizi wanazotumia watumishi wasio waaminifu katika hospitali za umma. Kufukuzwa kazi kwa Andrew Komba na Nelson Ileta, ambao pia walithibitika kutumia fomu batili za Mfuko wa Taifa wa

Kesi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) waliofukuzwa kwa kuwapa wagonjwa dozi kubwa za dawa kuliko mahitaji, wakitumia jina la daktari “hewa”, imeanika mbinu za wizi wanazotumia watumishi wasio waaminifu katika hospitali za umma.

Kufukuzwa kazi kwa Andrew Komba na Nelson Ileta, ambao pia walithibitika kutumia fomu batili za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kuwapa wagonjwa aina zaidi ya moja ya dawa kutibu ugonjwa wa aina moja kinyume na taratibu za kitabibu, ni kengele ya kuistua NHIF kuanza kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa madai.

Hivi karibuni Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) ilitengua uamuzi wa Tume ya Upatanishi na Uamuzi (CMA) wa kuwarejesha wafanyakazi hao kazini na kutaka walipwe stahiki zote walizostahili tangu walipofukuzwa kazi Februari, 2016.

Uamuzi huo ulitokana na ombi la Hospitali ya Muhimbili kutaka mahakama ipitie upya uamuzi wa CMA wa Mei 2018 ambao pia ulisema wafanyakazi hao walifukuzwa bila ya sababu za msingi.

Jaji Imani Aboud amesema katika uamuzi wake kuwa amejiridhisha kuwa MNH ilikuwa na sababu halali na za kutosha kuwaondoa watumishi hao kazini, licha ya ukweli kuwa hospitali hiyo ilikiuka utaratibu wa kisheria kuwaondoa katika ajira.

“Niseme tu katika shauri hili mahakama ingetamani wajibu maombi (watumishi waliofukuzwa) wasipate fidia yoyote kwa sababu kuna sababu halali za kufukuzwa kwao; wametenda kosa kubwa la kitaalauma,” alisema Jaji Aboud katika uamuzi wake.

“Hata hivyo, mikono yangu imefungwa kwa sababu sheria inatamka kwamba pale kusimamishwa kazi kunapokuwa si halali, iwe kwa sababu au taratibu, usimamishwaji huo unabaki kuwa wa makosa.”

Kutokana na kosa la kuwaondoa wafanyakazi hao kazini bila ya kufuata taratibu, Muhimbili italazimika kuwalipa mishahara ya miezi isiyozidi 12 bila kuwarudisha katika ajira zao.

Uozo waibuliwa

Komba na Ileta waliajiriwa na MNH mwaka 2010 na 2013 kama mfamasia mwandamizi na mfamasia kwa ajira za kudumu.

Mwezi Oktoba 2015 Muhimbili ililazimika kufanya uchunguzi wa kina baada ya kugundua kuwa dawa nyingi zilikuwa zikitolewa kwa kutumia jina la daktari aliyejulikana kwa jina la Alex ambaye hakuwemo katika orodha ya watumishi wa taasisi hiyo.

Watumishi hao wanadaiwa kutumia fomu batili za NHIF zilizosainiwa na Dk Alex kuwapa wagonjwa kiasi kikubwa cha dawa tofauti na mahitaji ya ugonjwa na pia kuwapa kwa wakati mmoja dawa za aina tofauti kutibu ugonjwa wa aina moja kinyume na taratibu za kitabibu.

Kufuatia kikao cha kamati ya nidhamu, wafanyakazi hao walikutwa na hatia na hatimaye kufukuzwa kazi Februari, 2016.

Mahakama yatofautiana na CMA

Komba na Ileta hawakuridhishwa na uamuzi wa kusimamishwa kazi na wakapeleka mgogoro huo CMA ambayo hatimaye Mei 2018 iliamuru warudishwe kazini na walipwe mishahara yote tangu siku waliposimamishwa kazi.

Uamuzi huo uliishitua Muhimbili ambayo iliamua kupeleka maombi ya kupinga uamuzi wa CMA.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, wakili wao Tumwesige Lushakuzi alidai kuwa MNH haikuwahi kutoa mbele ya CMA orodha rasmi ya madaktari wake kuthibitisha tuhuma kuwa madaktari walitoa dawa kwa kutumia jina la Dk Alex.

Alidai kuwa hospitali hiyo ilikuwa na wajibu wa kuwasilisha ushahidi kuwa Dk Alex hakuwemo katika orodha ya madaktari wa taasisi hiyo.

Pia alidai kuwa mashtaka kwamba wateja wake walifahamu kuhusu wingi wa dawa usio wa kawaida ulioidhinishwa katika fomu batili za NHIF kwa maslahi binafsi, hayakuthibitishwa CMA.

Kwa upande wake, wakili wa Muhimbili, Eneza Msuya ilisema wajibu wa wafamasia si tu kutoa kila dawa iliyoandikwa katika fomu ya daktari.

“Kama ingekuwa hivyo, basi kusingekuwa na haja ya kuwa na wafamasia walio na taaluma stahiki vya kitaaluma ili tu wawape wagonjwa chochote kilichoandikwa na daktari,” alidai.

Mwanasheria huyo alisema wafanyakazi hao walikuwa na wajibu wa kuhakikisha na kuthibitisha kile kilichoandikwa na daktari kabla ya kumpa mgojwa dawa.

Alisema fomu za NHIF zilizowasilishwa CMA zikiwa na jina la Dk Alex zisingeweza kufanyiwa kazi na mfamasia yeyote anayefanya kazi yake kwa kuzingatia maadili.

“Fomu hizo zilikuwa na makossa mengi. Zilielekeza kutolewa kiasi kikubwa cha dozi za dawa mbalimbali, zilielekeza kutolewa kwa dawa ambazo kitabitu hazipaswi kutolewa pamoja kwa matumizi ya aina moja ya ugonjwa na zilikuwa na mwandiko uliofanana.

“Mtaalamu yeyote wa ufamasia aliye makini na anayefanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yake, asingeweza kuzifanyia kazi,” alisema wakili huyo.

Ripoti ya kamati ya nidhamu ya MNH ilidhihirisha kuwa fomu zote batili za NHIF zilishughulikiwa na wafanyakazi hao.

Uamuzi CMA wamkera Jaji

Akitoa hukumu yake, Jaji Aboud alisema ameridhika kuwa Muhimbili imethibitisha kosa kubwa la kitaaluma dhidi ya wafanyakazi hao.

“Bila kusita, naona kuwa mleta maombi (MNH) alikuwa na sababu halali za kuwasimamisha kazi wajibu maombi (Komba na Ileta). Wajibu maombi, kama wafamasia, walikuwa na wajibu wa kutoa dozi kwa usahihi kwa wagonjwa bila kufungwa na maelekezo ya udanganyifu ya daktari hewa.

“Kama mwamuzi (CMA) angezingatia ipasavyo ushahidi katika rekodi, asingefanya uamuzi kwamba hakukuwa na sababu halali za kuwasimamisha kazi wajibu maombi,” alisema Jaji Aboud.

Hata hivyo, Jaji Aboud alisema kwa kiasi fulani Muhimbili haiwezi kukwepa lawama za kukiuka baadhi ya taratibu za kisheria za kuwasimamisha kazi watumishi hao, ikiwamo kutotoa wito wa kuwaita katika usikilizwaji wa shauri lao kwenye kamati ya maadili na kukiuka utaratibu wa kuwapa matokeo ya kikao hicho.

“Sina shaka kusema kwamba katika maombi yaliyo mbele yangu, licha ya sababu nzuri alizonazo mleta maombi kuwasimamisha kazi wajibu maombi, kwa bahati mbaya hakufuata baadhi ya taratibu za kisheria,” alisema Jaji Aboud.

“Sababu za kuwasimamisha kazi wajibu maombi zilikuwa halali, lakini taratibu hazikuwa sahihi. Wajibu maombi sasa watapata fidia kuwa kuondolewa kazini kinyume na taratibu.”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »