ZAIDI YA TSH.BILIONI 2.8 ZATUMIKA UNUNUZI WA VIFAA WEZESHI KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM 18,488 KOTE NCHINI.

ZAIDI YA TSH.BILIONI 2.8 ZATUMIKA UNUNUZI WA VIFAA WEZESHI KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM 18,488 KOTE NCHINI.

Barnabas Kisengi, Dodoma.Januari 14 ,2021 Katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora bila kujali hali aliyonayo,serikali imenunua vifaa wezeshi vyenye thamani  ya zaidi ya Tsh.Bilioni 2.8  vitakavyonufaisha wanafunzi wenye mahitaji Maalum 18,488 kote nchini. Akizungumza leo Januari 14,2021  katika zoezi la uzinduzi wa vifaa hivyo wezeshi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ,zoezi ambalo limefanyika Shule

Barnabas Kisengi, Dodoma.Januari 14 ,2021

Katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora bila kujali hali aliyonayo,serikali imenunua vifaa wezeshi vyenye thamani  ya zaidi ya Tsh.Bilioni 2.8  vitakavyonufaisha wanafunzi wenye mahitaji Maalum 18,488 kote nchini.

Akizungumza leo Januari 14,2021  katika zoezi la uzinduzi wa vifaa hivyo wezeshi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ,zoezi ambalo limefanyika Shule ya Sekoandari Dodoma,Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI]Seleman Jafo amesema   jumla ya vifaa Wezeshi 51,339  vimetolewa kwa watoto wenye mahitaji maalum 18,488 lengo ni kuhakikisha kila motto anapata elimu bora.

“Leo hii tukiwa tumekutana hapa ,katika ajenda hiyohiyo kuhakikisha suala la elimu linagusa kwa makundi yote ,ndio maana serikali mwaka 2018/2019 kutoa vifaa wezeshi kwa vijana wenye mahitaji maalum,mwaka huu pia  zaidi ya Tsh.Bilioni 2.8 imetumika katika ununuzi wa vifaa vipatavyo 51,339 lengo ni kuhakikisha ni kutengeneza mazingira wezeshi ya kupata elimu kwa watoto ambao kipindi kirefu walikuwa wakipata taabu suala la kupata elimu ni jambo la kumshukuru sana Mhe.Rais”amesema Jaffo

Aidha,Waziri Jafo amefafanua kuwa zaidi ya Tsh.Trioni 1.03 zimetolewa  na Serikali kwa ajili ya elimu bila malipo hadi  kufikia Mwishoni Mwa  Mwaka jana.

“Mhe.Rais kwa maelekezo yake ndani ya miaka mitano iliyopita na miaka hii mitano awamu yake ya  pili alielekeza elimu bila malipo zaidi ya Tsh.Bilioni 24 zinatolewa kila mwezi kwa lengo la kusaidia vijana wetu katika sekta ya elimu pamoja ujenzi wa miundombinu wezeshi ,hivyo mpaka tunamaliza mwka jana  zaidi ya Tsh.Trioni 1.03 zimetolewa  “amesema Jaffo

Hata hivyo ,Waziri Jafo amesisitiza utunzaji wa vifaa vipya vilivyotolewa ili viweze kusaidia wenye uhitaji kwa muda mrefu.

“Upatikanaji wa vifaa ni jambo moja na matumizi ya vifaa ni jambo lingine na wakati mwingine utunzaji wa vifaa ni jambo jingine na vifaa hivi ni vya kisasa sana ni jukumu la kila mmoja hasa walimu kuwa mstari wa   mbele katika utunzaji wa vifaa hivi na imani yetu kwamba vifaa hivi vitakuwa katika mazingira ya kisasa zaidi”amefafanua waziri Jaffo

Kwa upande katibu mkuu Ofisi ya Rais,TAMISEMI   Mhandisi Joseph Nyamhanaga amesema vifaa hivyo vinalenga kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiwemo Wenye ulemavu wa akili,ulemavu wa viungo,wasioona,viziwi,uoni hafifu ,ulemavu wa ngozi    huku akibainisha kuwa shule zinazohudumia wenye mahitaji maalum zimeongezeka kwa asilimia 46.1 % ikiwa  elimu ya Msingi  23.9%,sekondari ni asilimia 24.6%     .

“Jitihada za serikali ni pamoja na kuongezeka kwa shule zinazohudumia watoto wenye mahitaji maalum mbapo zimeongezeka hadi asilimia 46.1%”amesema Nyamuhanga

Aidha,Mhandisi Nyamhanga amebainisha idadi ya wanafunzi wenye ulemavu waliohitimu elimu ya msingi na kujiunga na elimu ya Sekondari imeongezeka kutoka asilimia 69.9%[wanafunzi 1117]kwa mwaka 2016 hadi asilimia 76.3%[Wanafunzi 2534 ]kwa mwaka 2020  huku bilioni 42.3 zimetumika kama chakula kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika kipindi cha miaka mitano.

Mkurugenzi anayeshughulikia  Elimu Maalum  Ofisi ya Rais ,TAMISEMI Julius Migeha  amesema serikali inaendesha zoezi la kubaini Watoto wenye mahitaji maalum katika kata zote 3956 kote nchini  ambapo ametoa wito kwa wazazi kutoa ushirikiano huku Mwanafunzi mwenye Mahitaji Maalum        Jackline Lazaro akitoa shukrani kwa kupata msaada huo.

Mkurugenzi anayeshughulikia  Elimu Maalum  Ofisi ya Rais ,TAMISEMI Julius Migeha  .

Vifaa Wezeshi hivyo jumla ni  51,339  vitasambazwa nchi nzima kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao ni jumla ya watoto 18,488 .

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »