MHE. HEMED AWAFARIJI WANA CCM WILAYA KUSINI KWA KUUNGULIWA NA MOTO KWA OFISI YAO

MHE. HEMED AWAFARIJI WANA CCM WILAYA KUSINI KWA KUUNGULIWA NA MOTO KWA OFISI YAO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wanachama wa CCM na Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja kuendelea kuwa watulivu na wastahamilivu katika kipindi hichi kifupi kufuatia Jengo la Afisi yao ya Chama Wilaya kuungua Moto.Mheshimiwa Hemed Suleiman ametoa kauli hiyo wakati alipozuru eneo la tukio hapo Makunduchi kuona athari


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wanachama wa CCM na Wananchi wa Wilaya ya Kusini Unguja kuendelea kuwa watulivu na wastahamilivu katika kipindi hichi kifupi kufuatia Jengo la Afisi yao ya Chama Wilaya kuungua Moto.
Mheshimiwa Hemed Suleiman ametoa kauli hiyo wakati alipozuru eneo la tukio hapo Makunduchi kuona athari halisi na kuwapa pole Wanachama hao pamoja na Wananchi wa Wilaya hiyo walioshirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na janga hi

 
Makamu wa Pili amesema Viongozi pamoja na Wananchi wa Mikoa mengine Nchini wanaelewa fika kwamba Mkoa wa Kusini unabakia kuwa ngome ya CCM kutoka na uimara wake ukilinganishwa na Mikoa mengine Hivyo, mikoa menngine inapaswa kufuata nyayo za Mkoa huo.
Mapema Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini Nd.Hafidh Hassan Mkadam amesema Taarifa za ajali hiyo ya Moto kwenye Jengo la Afisi ya CCM Wilaya ya Kusini walizipata majira ya saa 12.20 jioni na kufika eneo la tukio muda huo huo.


Nd. Hafidh amemueleza Mheshimiwa Hemed Suleiman kwamba harakati za kunusuru Mali na vifaa vilivyomo ndani ya Ofisi za Jengo zilizounganisha nguvu za Wana CCM na Wananchi wa eneo hilo bila ya kujali Itikadi zao za Kisiasa ziliweza kuokoa vifaa vichahe ikiwemo mashine ya Fotokopi.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amekutana na Timu ya Viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege ya Favori  kutoka Nchini Uturuki.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mheshimiwa Hemed Suleiman ameueleza Ujumbe huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshafungua milango wazi katika kukaribisha fursa za Uwekezaji Visiwani Zanzibar.
Mapema Viongozi hao wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Miundombinu ya Ujenzi wa Viwanja vya Ndege ya Favori kutoka Nchini Uturuki  ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Bora Isiner amesema Kampuni yao imeridhika na mazingira halisi ya Uwekezaji yaliyopo Zanzibar.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)Januari 14, 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »