Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalazimika kuendelea kuwaheshimu Wasanii Nchini kutokana na mchango wao mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa Jamii na Taifa kwa jumla katika suala zima la kufikisha Ujumbe, Elimu sambamba na burdani. Akizungumza na Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Kizazi Kipya {ZFU} waliofika Afisini kwake Vuga kujitambulisha, Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalazimika kuendelea kuwaheshimu Wasanii Nchini kutokana na mchango wao mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa Jamii na Taifa kwa jumla katika suala zima la kufikisha Ujumbe, Elimu sambamba na burdani.
Akizungumza na Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Kizazi Kipya {ZFU} waliofika Afisini kwake Vuga kujitambulisha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla amesema Zanzibar kipindi hichi inapaswa kurejea katika hadhi yake ya kuibua Wasanii waliobobea katika anga za Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Uongozi huo wa Chama cha Wasanii wa Kizazi Kipya amewatoa hofu Wasanii Nchini kwamba wajiandae kushirikishwa katika shughuli zozote za Kitaifa wakati zinapofanyika iwe Mjini au Vijijini na wakati mwengine hata Tanzania Bara jambo ambalo huwa likifanyika.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Wasanii wa Kizazi Kipya Zanzibar Makame Mshimba Mbarouk amesema Wasanii wachanga Nchini wameomba kupewa fursa ya kuvitumia vipaji vyao katika kufikisha Ujumbe na kutoa Burdani kwa Jamii mahala popote watakapopangiwa.
Naye kwa upande wake Rais wa Chama cha Wasanii wa Kizazi Kipya Mohamed Abdulla Laki ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake maalum wa kuwashirikisha Wasanii na Wanamichezo kwenye Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar za Mwaka huu zilizofikia Kilele chake katika Uwanja wa Mnazi Mmoja.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR) Januari 14, 2021.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *