MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA AFANYA ZIARA YA KIKAZI JIMBONI KWAKE.

MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA AFANYA ZIARA YA KIKAZI JIMBONI KWAKE.

Alhamisi 14 Januari 2021, Mbunge wa jimbo la Segerea *Mh. Bonnah Ladislaus Kamoli (MB)* amefanya ziara ya kikazi katika kata za Kinyerezi, Bonyokwa, Kisukuru na Segerea. Katika ziara hii *Mh. Bonnah* aliongozana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala *Ndugu Jumanne Shauri* pamona na wahandisi wa manispaa ya Ilala ambao ni wakuu wa Idara za TARURA


Alhamisi 14 Januari 2021, Mbunge wa jimbo la Segerea *Mh. Bonnah Ladislaus Kamoli (MB)* amefanya ziara ya kikazi katika kata za Kinyerezi, Bonyokwa, Kisukuru na Segerea.

Katika ziara hii *Mh. Bonnah* aliongozana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala *Ndugu Jumanne Shauri* pamona na wahandisi wa manispaa ya Ilala ambao ni wakuu wa Idara za TARURA na DMDP, Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi Wilaya ya Ilala *Comrade Said Sultan Sidde*, Waheshimiwa madiwani wa kata husika pamoja na viongozi wa chama na serikali wa kata husika.

Malengo ya ziara hii yalikuwa ni kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kata za Kinyerezi na Bonyokwa ambayo yameongezwa ili kupokea wanafunzi wa kidato Cha kwanza waliokuwa wameachwa kutokana na uhaba wa madarasa ila wametakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa siku chache zilizopita.

Lakini pia kukagua miundombinu ya barabara ambayo ujenzi wake unahitaji udharura wa kipekee.

Katika kata ya Kinyerezi, Mh. Mbunge pamoja na msafara alioambatana nao alipokelewa na diwani wa kata hiyo *Mh. Leah M* na walikagua ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya Sekondari Kinyerezi Annex. Vyumba viwili Kati ya hivyo tayari vimepauliwa na ujenzi wake unakadiliwa kukamilika Kabla ya tarehe 25 January mwaka huu. Vyumba vitatu vipo kwenye msingi. Hivi navyo ujenzi wake unakadiliwa kukamilika February 26.

Diwani wa kata ya Bonyokwa *Mh. Tumike Malilo* Akiongoza msafara wa Mh. Mbunge na alioambatana nao, walizuru barabara ya zahanati ya Bonyokwa ambayo imeharibika vibaya.

Mh. Bonnah* alimueleza Mkurugenzi juu ya umuhimu wa barabara hii. Lakini namna ambavyo wananchi wanasumbuka hasa wagonjwa hususani wamama wajawazito kwani hata gari la kubebea wagonjwa (ambulance) halina pakupita inapotokea dhalura ya kuhitajika kwake. Mkurugenzi amewaagiza TARURA kuhakikisha wanaikarabati kwa kiwango Cha zege Mara Moja barabara hiyo. Huku akiahidi kuwapatia ushirikiano wa hali na Mali wakiuhitaji.

Baada ya zahanati ziara iliendelea kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Bonyokwa. Vyumba sita vya madarasa vinajengwa na ujenzi wake unakadiliwa kukamilika February 20 mwaka huu. Pamoja na mradi huu Mkuu wa shule amemueleza Mkurugenzi juu ya ukosefu wa Choo cha walimu. Mkurugenzi ameahidi kutatua tatizo la ukosefu wa choo hicho lililokuwa linaikumba shule hii Mara Moja huku akisema kuwa Kabla ujenzi wa vyumba vya madarasa haujaisha basi huenda na ujenzi wa Choo ukawa umeanza.

Katika kata ya Kisukuru, Diwani wa kata hii *Mh. Lucy Lugome* aliuongoza msafara wa mbunge kuona madaraja ya *Maji chumvi na Migombani* ambayo yako katika hali mbaya na Daraja la Migombani likiwa limekatika kabisa hivyo kukatisha mawasiliano Kati ya wananchi wa Manzini ni mitaa mingine na hasa kusababisha adha ya watoto kwenda shule. Mkurugenzi ameagiza kuanzia Jumatatu 18 January kazi ya kukarabati madaraja haya ianze ili kurudisha mawasiliano huku wakiwa wanajipanga kutafuta suruhisho la kudumu.

Ziara iliendelea katika kata ya Segerea ambako diwani wa kata hiyo *Mh. Robert Manangwa* aliuongoza msafara wa Mh. Mbunge kwenda kuona barabara ya Kwa Bibi kwenda Zahanati na Ile ya Chama kwenda Segerea Kusini. Mkurugenzi amewaagiza wahandisi kuona namna ya kufanya ili ukarabati wa barabara hizi ufanyike haraka.

Akitoa maneno ya shukrani kwa Mkurugenzi *Mh. Bonnah* alimshukuru sana kwa namna alivyotoa maamuzi yatakayopelekea utatuzi wa changamoto walizokutana nazo katika ziara, lakini kwa kutenga muda wake na kwenda site kujionea hali halisi ya changamoto anazowasilishiwa.

Naye *Mkurugenzi* amempongeza Mh. Mbunge kwa namna anavyo pambana ili kuwaondolea kero wananchi wake. Amemuahidi ushirikiano wa kuendelea kufanya ziara hizi katika kata zingine kwa kadri atakavyohitajaika. Amewasisitiza wakandarasi waliopewa Kazi za ujenzi wowote iwe ni vyumba vya madarasa au barabara kuhakikisha wanakamilisha kazi zao kama mikataba inavyowataka na pengine Kabla ya hapo.

Naye *Comrade Said Sultan Sidde* Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi wa Wilaya ya Ilala. Amempongeza *Mh. Bonnah* na madiwani kwa ushirikiano wanaouonesha katika kuisimamia Serikali ili itekeleze kilichoaahidiwa katika ILANI ya uchaguzi ya CCM ya 2020/2025. amempongeza pia Mkurugenzi kwa kuhakikisha anatoka yeye mwenyewe ofisini na kwenda kuitika wito wa mbunge wa kutatua kero za wanasegerea.

Ziara hizi hasa za kuona barabara kurofi na zinazohitaji matengenezo ya dhalura Jimboni Segerea zimeanza rasmi na *Mheshimiwa Mbunge* atapita Kata kwa kata na mtaa kwa mtaa yeye mwenyewe aliongozana na viongozi wa serikali waliopewa Kazi ya kutatua changamoto za wananchi. 
Imeandaliwa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Segerea.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »