Jumla ya Wainjilisti wa vitabu 798 kanisa la Waadventista Wasabato watunukiwa vyeti vya Utumishi.

Jumla ya Wainjilisti wa vitabu 798 kanisa la Waadventista Wasabato watunukiwa vyeti vya Utumishi.

Na Barnabas kisengi Kahama Shinyanga.January 31 2021 Katika kuendelea kusongesha mbele  kazi ya utume,Jumla ya wainjilisti wa vitabu 798 kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la Nyanza ukanda wa dhahabu- Nyanza Gold Belt Field(NGBF) wametunukiwa vyeti kutokana na kazi nzuri ya usambazaji wa vitabu vya utume. Akizungumza leo January 31,2021  katika hitimisho la kambi la pamoja

Na Barnabas kisengi Kahama Shinyanga.January 31 2021


Katika kuendelea kusongesha mbele  kazi ya utume,Jumla ya wainjilisti wa vitabu 798 kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la Nyanza ukanda wa dhahabu- Nyanza Gold Belt Field(NGBF) wametunukiwa vyeti kutokana na kazi nzuri ya usambazaji wa vitabu vya utume.


Akizungumza leo January 31,2021  katika hitimisho la kambi la pamoja la uinjilisti wa vitabu jimbo la Nyanza,ukanda wa Dhahabu (NGBF) Askofu Mkuu kanisa la waadventista wasabato jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania Mchungaji na Daktari  Godwin Lekundayo amesema kitabu ni mjumbe mwenye uchungu wa kwenda kuikomboa dunia iliyoangamia lakini havina miguu hivyo ametoa wito kwa washiriki kuwashika mkono wainjilisti hao ili waweze kufikisha vitabu katika maeneo mbalimbali.


Mchungaji na Daktari Lekundayo amesema maelfu ya watu ambao wanapeleka ujumbe wa vitabu katika maeneo mbalimbali wamekuwa na msaada mkubwa katika kuukomboa ulimwengu uliojaa maovu hivyo wainjilisti wa vitabu ni moja ya njia sahihi ya upelekaji wa injili.


Aidha,Askofu Lekundayo ametoa wito kwa vijana hususan wasomi kufanya kazi kwa bidii na kuacha uzembe  ambapo amebainisha kuwa Mungu haiti watu ambao ni wazembe na legelege wanaokaa tu vijiweni  hivyo ni wajibu kwa kila kijana kufanya kazi  .

Ameendelea kufafanua kuwa ni jambo la kuumiza vijana wasomi na wamehitimu fani mbalimbali na wamekaa tu badala ya kufanya kazi ya Mungu pamoja na kazi yoyote halali ya kuwaingizia kipato.


Sanjari na hayo Mchungaji na Daktari Lekundayo amebainisha kuwa sisi kama Wakristo hatupaswi  kubagua mtu na kusema ni mlevi sana hatoingia mbinguni kwani Mungu anajua watu wake na kila mtu anafaa kwa Muumba hata kama ni muovu namna gani..Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jimbo la Nyanza ,Ukanda wa Dhahabu,Kanisa la Waadventista Wasabato (NGBF) Mchungaji Enock Sando amesema kambi hilo wa Wainjilisti wa Vitabu limekuwa na mibaraka tele katika kuhamasisha upelekaji wa vitabu vya utume katika maeneo ya hospitalini,magerezani,mtaani na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Kwa upande wao baadhi ya Wainjilisti wa vitabu akiwemo Neema Lameck kutoka Ushirombo amesema kambi hilo limewapa msukumo zaidi wa wa upelekaji wa vitabu wa utume …Kambi la pamoja la Wainjilisti wa vitabu limefanyika katika kanisa la Waadventista Wasabato Nyahanga Manispaa ya Kahama  ambapo limevuka malengo ya kutunuku  vyeti kutoka wainjilisti 600 hadi wainjilisti 798. 


Hivyo kambi hilo limekutanisha wainjilisti kutoka Kahama ,Geita,Ushirombo,Masumbwe,Kakola na Katoro neno kuu likiwa ni “Nitakwenda nilete Matumaini kwa kila Nyumba

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »