Bryan Mosses:Waandishi wa habari hakikisheni mnachukua tahadhari ya kujikinga na corona katika maeneo yenu ya kazi.

Bryan Mosses:Waandishi wa habari hakikisheni mnachukua tahadhari ya kujikinga na corona katika maeneo yenu ya kazi.

Na Barnabas kisengi Dodoma February  01  2021 Wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dodoma CPC wametakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya kwa kuhakikisha wanafuata kanuni na sharia ya afya katika kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa wa covid 19 ambao bado unasumbua dunia kwa ujumla Wito huo umetolewa jijini Dodoma na mwandishi wa

Na Barnabas kisengi Dodoma February  01  2021


Wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dodoma CPC wametakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya kwa kuhakikisha wanafuata kanuni na sharia ya afya katika kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa wa covid 19 ambao bado unasumbua dunia kwa ujumla

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na mwandishi wa habari wa kituo cha Sahara media Bryan Mosses wakati kuzungumza na Jfive one line blog juu ya hali ya ugonjwa wa covid 19 (corona)  ambao ugonjwa huo bado upo na unasumbua dunia  hivyo twapaswa kuendeleakuchukua tahadhari kila wakati ili kujikinga na janga hili


“kwa waandishi wenzangu hakikisheni mnapokuwa kwenye majukumu yenu ya kila siku hakikisheni mnafuata taratibu za wizara ya afya kwa kuwa mnanawa mikono mara kwa mara nakuhakikisha mnatumia sabuni kila mara na kwa maeneo ya mikusanyiko mhakikishe mnakuwa makini kwa kujitahadhari na ugonjwa huu”amesema Bryan mosses


“pia Kama waandishi sasa ifike wakati kwa kutumiwa kalamu zenu mnahakikisha mnatoa mchango wa elimu kwa jamii nzima hapa nchini kuwapa elimu ya kujikinga na ugonjwa huu katika kipindi hichi ambacho ugonjwa huu bado unatusumbua”


Waandishi ndio kioo cha jamii hivyo mkiwa mnaonyesha mfano wa kujikinga na magonjwa haya kwa wananchi ni rahisi kuiga mifano kutoka kwetu hivyo tuhakikishe katika Nyumba zetu, ofisini kwetu tunaweka vifaa vya kutakasa mikono kwa kuweka maji tiririka na sabuni ili kuhakikisha tunakuwa mfano wa kwanza kwa kujikinga na magonjwa haya

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »