WIZARA YA AFYA HAINA MPANGO WA KUPOKEA CHANJO YA Covid19 .Dkt. Gwajima.

WIZARA YA AFYA HAINA MPANGO WA KUPOKEA CHANJO YA Covid19 .Dkt. Gwajima.

Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imetoa rasmi ufafanuzi wa namna ya kutengeneza dawa ya kunywa na kupiga nyungu ili kujikinga na magonjwa mbalimbali na kuwataka wananchi kuzitumia dawa hizo asili ili kujilinda na magonjwa mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari Mosi, 2021 jijini Dodoma Waziri wa Afya,

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Godwin Mollel wakinywa dawa ya kujikinga na magonjwa mbalimbali mbele ya waandishi wa habari.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima akipiga nyungu mbele ya waandishi wa habari.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Godwin Mollel akipiga nyungu mbele ya waandishi wa habari.

Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imetoa rasmi ufafanuzi wa namna ya kutengeneza dawa ya kunywa na kupiga nyungu ili kujikinga na magonjwa mbalimbali na kuwataka wananchi kuzitumia dawa hizo asili ili kujilinda na magonjwa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari Mosi, 2021 jijini Dodoma Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima amesema madhumuni ya ufafanuzi huo ni juu ya maswali kadhaa ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wanahabari ambao wamekuwa wakimuuliza kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

“Kufuatia taarifa za uwepo wa mlipuko wa pili wa ugonjwa wa corona, Covid19 katika nchi jirani nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa wanahabari.amesema Dkt.Gwajima.


“Wizara ya Afya haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine, ifahamike kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya inayo taratibu za kufuata pale inapotaka kupokea bidhaa yoyote ya afya baada ya Serikali kujiridhisha hivyo kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe na si vinginevyo,” amesema Dk Gwajima.

Aidha Dkt Gwajima amesema wizara inaendelea kuwakumbusha wananchi mbinu mbalimbali za kujikinga na ugonjwa huu kwa kujielekeza kwenye elimu ambayo imekuwa ikitolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuimarisha usafi wa manyumbani na mtu binafsi kuwa msafi wakati wote,kujifukizia,kufanya mazoezi, kula Lishe bora, kunywa maji mengi na bila kusahau matumizi ya tiba asili ambazo taifa letu la Tanzania limejaliwa
Dkt Gwajima amesema wizara kwa kushirikiana na mkemia mkuu wa serikali na baraza la tiba asili na wananchi wajuzi wa tiba asili tayari wameshafanya usajili wa bidaa (dawa) za tiba asili miongoni mwao dawa ya covidol ambayo imekuwa ikiwasaidia Sana wagonjwa wanaiugua magonjwa mbalimbali ikiwemo haya ya mfumo wa hewa
“Elimu ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na matumizi ya tiba asili itaendelea kutolewa na wataalamu wetu wa afya sambamba na mimi waziri na naibu waziri ambao kitaaluma sisi ni madaktari wa binadamu tukianza kujikinga Sisi na viongozi wengine na wananchi wote kutekeleza kwa vitendo matumizi ya mbinu za kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza ikiwemo kufanya mazoezi katika mitaa yetu na Nyumba zetu kufanya usafi wa maeneo tunayoishi kunywa maji mengi kufanya usafi wa miili yetu kula chakula bora kujifukizia na kutumiwa tiba asili hakika tutaweza kujinusuru na magonjwa haya”amesema Dkt Gwajima.

Na Barnabas kisengi Dodoma.

February  01 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »