Ziara ya Mstahiki Meya wa Ilala katika Kata ya Upanga Magharibi na kata ya Buguruni

Ziara ya Mstahiki Meya wa Ilala katika Kata ya Upanga Magharibi na kata ya Buguruni

Na Barnabas kisengi Dar es salaamFebruary  10  2021 Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto amefanya ziara yake ya kikazi katika Kata ya Upanga Magharibi pamoja na Kata ya Buguruni katika ziara hiyo Mstahiki aliambatana na Afisa Elimu Manispaa ya Ilala Mwalimu Mussa. Katika Kata ya Upanga Magharibi Mstahiki alitembelea Ujenzi wa Bweni katika

Na Barnabas kisengi Dar es salaamFebruary  10  2021


Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto amefanya ziara yake ya kikazi katika Kata ya Upanga Magharibi pamoja na Kata ya Buguruni katika ziara hiyo Mstahiki aliambatana na Afisa Elimu Manispaa ya Ilala Mwalimu Mussa.


Katika Kata ya Upanga Magharibi Mstahiki alitembelea Ujenzi wa Bweni katika Shule ya Secondary ya Wavulana Azania. Mstahiki amejionea Ujenzi wa Bweni lakini hajaridhishwa na mwenendo wa Ujenzi wa Jengo hilo.”Speed ya Kazi imekuwa ndogo sana, mafundi wapo wachache, hapa Mkandarasi unatakiwa kuongeza mafundi lakini pia ikiwezekana kazi ifanyike usiku na mchana ili kukamilisha hili jengo kwa wakati” Amesema Mstahiki Meya


Mstahiki Meya alimalizia ziara  kwa kufikisha salamu za Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azan Zungu ambaye kwa sasa yupo kwenye vikao vya Bunge Dodoma.
Katika Kata ya Buguruni Mhe Kumbilamoto alitembelea eneo la Gereji ambapo Serikali inampango wa kujenga Shule ya Secondary ya Gorofa itahudumia Kata ya Buguruni pamoja na Kata za jirani, Changamoto inayokwamisha ujenzi huwo ni bajeti ya kuchimb kiasi cha mita 10 kuondoa udogo mchafu ili ujenzi uanze, Eneo hilo zamani lilikuwa likitumika kama dampo. Mstahiki Meya amelipokea na kuahidi kwenda kulifanyia kazi. Eneo hili likifanikiwa Kata ya Buguruni itakuwa na jumla ya Shule mbili za Secondary na itapunguza idadi kubwa ya wanafunzi katika baadhi ya Shule.

Katika Shule ya Secondary Buguruni Moto Mhe. Kumbilamoto amezungumza na wafanya biashara ndogo ndogo ambao wamejenga mabanda ya biashara katika eneo la Shule kuvunja na kujenga pembeni mwa majengo ya Shule.


” Kwasasa tumekwama kupata usajili kutoka Tamisemi kwaajili ya Shule hii kutokana na madarasa kuwa karibu na mabanda ya biashara, Hivyo mabanda haya ambayo yamejengwa hapa yavunje na yajengwe nje ya eneo la Shule nami nachangia shilingi 100,000/= kwaajili ya ubomoaji wa  mabanda hayo.” Amesema Mstahiki Meya
Mwisho Mstahiki Meya alifikisha salama za Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe Bonnah kwa wananchi na wafanya biashara katika Eneo hilo la Buguruni Moto.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »