IBADA YA KUAGA MWILI WA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI.

IBADA YA KUAGA MWILI WA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI.

PICHA MBALIMBALI ZA IBADA YA KUAGA MWILI WA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA. Mwili wa marehemu Mhandisi Balozi John William Kijazi aliyekuwa katibu mkuu kiongozi (ikulu)  na mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)  umeagwa leo jijini Dodoma katika eneo la chuo kikuu cha Dodoma na kusafirishwa kuelekea mkoani

PICHA MBALIMBALI ZA IBADA YA KUAGA MWILI WA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA.

Mwili wa marehemu Mhandisi Balozi John William Kijazi aliyekuwa katibu mkuu kiongozi (ikulu)  na mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)  umeagwa leo jijini Dodoma katika eneo la chuo kikuu cha Dodoma na kusafirishwa kuelekea mkoani Dar es salam ambapo unatarajiwa kuagwa kesho kitaifa ambapo Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania anategemewa kuongoza Salam za kuuaga mwili huo kabla ya kusafirishwa kuelekea mkoani Tanga wilaya ya korogwe Ambapo marehemu mhandisi balozi John William kijazi atazikwa wilayani korogwe
Akiongoza salamu za serikali katika kuuaga mwili huo jijini Dodoma waziri wa elimu sayansi tekinolojia na ufundi mh ndalichako amesema watamkumbuka Sana Balozi kijazi kwa utumishi uliotukuka katika utendaji wake wa kazi kwakuwa Alikuwa mkulugenzi anayependa kusikiliza kwanza na ndio akupeushauri wake pia alikuwa hana makundi ya viongozi wala upendeleo wowote kwa mawaziri wala makatibu wakuu
Aidha ndalichako amesema Alikuwa mshauri wa rais wa karibu sana na amemshauri vizuri rais hadi sasa alipopoteza uhai wake jana usiku tumepata pigo kubwa na pengo kubwa kwa sisi mawaziri makatibu wakuu na haswa kwa Mh rais amepita pengo kubwa Sana katika utendaji wa kazi wa marehemu mhandisi balozi John kijazi tunamuombea mwenyezi mungu ampumzishe Mahalia pema peponi
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Bilthi mahenge akitoa salamu za mkoa wa Dodoma amesema mkoa utamkumbuka Sana kwani marehemu mhandisi balozi kijazi ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa kuratibu na kuhakikisha makao mkuu yamehamia hapa Dodoma na amekuwa mshauri mkubwa katika kuratibu shughuli zote ambazo hadi sasa mnaiyona Dodoma imekamilika kuwa makao makuu hizo zote ni jitihada za marehemu kijazi kwa kumshauri rais vizuri
“kwakweli marehemu kijazi ametutendea mema wana Dodoma kwa kuhakikisha makao makuu imekamilika na ameratibu watumishi wote kuhakikisha wamehamia Dodoma na mawaziri na makatibu wakuu hakika tumepata pengo kubwa wana Dodoma kubwa ni kuendelea kumwombea huko aliko maana marehemu kijazi hakuwa mtu wa kujikweza kutokana na nafasi yake kwa sisi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya alituchukulia kama ndugu tulio sawa pamoja na mapungufu yetu ya kibinadamu tunamwombea apumzike salama huko aliko”amesema mkuu wa mkoa wa Dodoma 
Marehemu mhandisi balozi John kijazi enzi za uhai wake Alikuwa katibu mkuu kiongozi ikulu na mkuu wa chuo cha Dodoma alizaliwa 1956 na kukutwa nayumauti February 17 majira ya sasa 3 na dakika 10 katika hospitali ya Benjamin mkapa iliyoko chuo kikuu cha Dodoma udom na marehemu kijazi ameacha mjane moja na watoto watatu wa kiume mwili wa marehemu balozi John William kijazi umesafirishwa kwa Ndege kuelekea mkoani dar es salaam ambapo kesho utaagwa kitaifa na kuelekea mkoani tanga wilayani korogwe kwa mazishi yatakayofanyika siku ya jumamosi. 
“Raha ya milele uumpe ebwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani” amina

Na Barnabas kisengi Dodoma.

 February 18 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »