Takukuru ya ibana Kampuni ya GENEVA CREDIT SHOP ya riba umiza ya Abubakari Mapesa kuwalipa walimu wastaafu zaidi ya shilingi milioni 176.

Takukuru ya ibana Kampuni ya GENEVA CREDIT SHOP ya riba umiza ya Abubakari Mapesa kuwalipa walimu wastaafu zaidi ya shilingi milioni 176.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imetoa wito kwa wakopeshaji wa fedha Mkoani hapa kuzingatia Kanuni na taratibu za nchi na kuacha tabia ya kuwatoza wananchi riba umiza.Wito huo unatolewa na Taasisi hiyo baada ya kurejesha jumla ya fedha shilingi milioni 176,565,000 kwa wananchi wanyonge waliodhurumiwa wengi wao wakiwa ni

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imetoa wito kwa wakopeshaji wa fedha Mkoani hapa kuzingatia Kanuni na taratibu za nchi na kuacha tabia ya kuwatoza wananchi riba umiza.
Wito huo unatolewa na Taasisi hiyo baada ya kurejesha jumla ya fedha shilingi milioni 176,565,000 kwa wananchi wanyonge waliodhurumiwa wengi wao wakiwa ni walimu wastaafu na kampuni ya GENEVA CREDIT SHOP inayomilikiwa ba Bwana Abubakari Kinyuma maarufu kama Abubakari Mapesa iliyopo Mjini kondoa Mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoani hapa Bwana Sosthenes Kibwengo amesema baada ya kufanyia uchunguzi Kampuni hiyo mwezi januari 2021walibaini kuwa mmiliki wa Kampuni hiyo hukopesha fedha kwa riba kubwa ambapo imepelekea wananchi kumlalamikia kutoka na mikopo umiza anayoitoa.

Aidha amesema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wataendelea kukokota kiasi cha kodi ambacho Kampuni hiyo inadaiwa huku ikiendelea kufuatilia shilingi milioni 184,586,000 za wakopeshaji 22 ambazo zinapaswa kurejeshwa na Bwana mapesa .

Wakizungumza Mara baada ya kurejeshwa fedha zao ,wananchi hao wameishukuru Taasisi hiyo kwa kuwasaidia kupata fedha zao ambazo zilichukuliwa na Bwana Mapesa kwa kuongezeka riba kubwa .

Hatahivyo, wananchi wamekumbwa kujihadhari na mikopo umiza na kamwa wasikubali kumkabidhi kadi zao za benki kwa mtu yeyote

Na Barnabas kisengi Dodoma.

 February  18 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »