Watoto 70 Kati ya 176 wamepatiwa huduma ya matibabu ya utapiamlo mkali wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Watoto 70 Kati ya 176 wamepatiwa huduma ya matibabu ya utapiamlo mkali wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Halimashauri ya wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma kwa kipindi cha October 2020 hadi sasa  2021 jumla ya watoto 70 Kati ya 176 wamepatiwa huduma ya matibabu ya utapiamlo mkali ili kupunguza vifo vya watoto wadogo vinavyotokana na Lishe duni huku kwa kipindi hicho jumla ya wakinamama wajawazito 8670 Kati ya  10197 wamepatiwa elimu ya Lishe


Halimashauri ya wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma kwa kipindi cha October 2020 hadi sasa  2021 jumla ya watoto 70 Kati ya 176 wamepatiwa huduma ya matibabu ya utapiamlo mkali ili kupunguza vifo vya watoto wadogo vinavyotokana na Lishe duni huku kwa kipindi hicho jumla ya wakinamama wajawazito 8670 Kati ya  10197 wamepatiwa elimu ya Lishe bora na vidonge vya kuongeza damu vinavyopatikana katika maeneo yao ambavyo vinaongeza damu kwa wino na kuwaelekeza wakina mama wajawazito kufuata tabia chanya ambazo zinaboresha ulaji na virutubishi kwa ufanisi katika kipindi chote cha ujauzito wao.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa afua ya Lishe katika kikao kazi cha kamati ya Lishe ya halimashauri ya wilaya ya mpwapwa Afisa Lishe wilaya Renatus Komba amesema bado kunachangamoto kubwa ya akina mama wengi wajawazito kutohudhuria kliniki kwa kipindi hichi kwa kusingizia wako katika palizi baada ya kulima mazao yao jambo ambalo huatarisha maisha kwa kuto kuto kwenda kliniki kwa wakati
Renatus komba amesema Kama kamati ya Lishe wilaya wameweka mikakati kupita halimashauri hiyo ikiwemo kutoa elimu kwa wajawazito na wakina mama wilayani mpwapwa pia halimashauri imeendelea kutenga na kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za Lishe na kuenddelea kutoa elimu na kuwafikia watu wengi zaidi katika utekelezaji wa afua za Lishe kwa ngazi ya kaya,vitongoji,vijiji na Kata kwa kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani hapo. 
Aidha Renatus komba amesema halimashauri ya wilaya ya mpwapwa imefanikiwa kuwawezeha wajumbe wa kamati ya Lishe kufanya ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa usimamizi shirikishi wa kukagua na kuona afua za Lishe katika vituo vya kutolea huduma za afya jamii ya msingi na kutembelea ofisi za serikali za vitongoji, vijiji na mitaa katika Kata 28 kati ya Kata 33 na kuzungumza na watoa huduma katika maeneo yao na kuzungumza na wajawazito katika maeneo yote waliyofanikiwa kufika katika ziara hiyo. 
Pai afisa Lishe Renatus komba amebainisha mafanikio mengine yaliyotolewa na halimashauri kwa kushirikiana na wadau wa Lishe wameweza kufanikiwa kufanya maonyesho ya Lishe bora katika vijiji 63 kwa lengo la kuwaelekeza jamii na akina mama wajawazito kutumia Lishe bora ya vyakula mchanganyiko vinavyopatikana katika maeneo yao wanayoishi kwa kutengeneza Lishe kwa watoto wanaoanza kula na wamefanikiwa kuwapa elimu wakinamama 775 walio katika umri wa kuzaa walipatiwa elimu hiyo. 
“Ninaona umuhimu wa kamati ya Lishe ya wilaya kwakuwa inakuwa inafanya ufuatiliaji wa karibu kwa walengwa na kwa halimashauri na mabadiliko yameanza kuonekana hapa wilayani kubwa ni kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Lishe katika kutoa elimu kwa jamii yetu ili tuweze kupunguza vifo vya watoto na kuondokana na utapiamlo mkali hapa wilayani kwetu kwa kushirikisha makundi mbalimbali na kamati ya Lishe”alisisitiza Renatus komba
Awali akifungua kikao hicho cha kamati ya Lishe wilaya mwenyekiti wa kamati ya Lishe wilaya Paulo sweya ambaye pia ni mkulugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo amesema halimashauri inaendelea kutoa huduma kwa kuhakikisha miongozo yote inayotolewa na serikali kuhusu Lishe inatekeleza maelekezo na maagizo hayo kwa wakati na kuendelea kutenga bajeti ya Lishe katika maeneo yote yaliyoelekezwa pia kuwashirikisha madiwani wa Kata zote katika vikao vya baraza la madiwani wilayani hapo. 

Na Barnabas kisengi Mpwapwa.

 February 20  2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »