Na Barnabas kisengi Dodoma February 24 2021 WAZIRI wa Afya,maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto,Dorothy Gwajima amemuagiza Katibu Mkuu,Idara kuu ya maendeleo ya Jamii kuhakikisha anampatia taarifa kuhusu Fedha zinazotolewa na Serikali kupitia halmashauri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi. Hatua hiyo ya Waziri Gwajima imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kuwa hawajapata mikopo ambayo imekuwa ikitolewa na
Na Barnabas kisengi Dodoma
February 24 2021
WAZIRI wa Afya,maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto,Dorothy Gwajima amemuagiza Katibu Mkuu,Idara kuu ya maendeleo ya Jamii kuhakikisha anampatia taarifa kuhusu Fedha zinazotolewa na Serikali kupitia halmashauri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Hatua hiyo ya Waziri Gwajima imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kuwa hawajapata mikopo ambayo imekuwa ikitolewa na Serikali katika kuwawezeshakiuchumi huku wengine wakidai hawajui kama kuna Fedha hizo.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya jamii DECOPATA lenye Lengo la kuboresha utendaji kazi ambalo limewashirikisha maafisa wa maendeleo ya jamii Nchini pamoja na wataalam wa maendeleo ya Jamii.
Hata hivyo amebainisha kuwa dhamira ya Serikali ni kuiwezesha Tanzania ifikapo2025 iwe Nchi ya uchumi wa Kati ambapo jitihada za uwezeshaji wananchi kiuchumi hivi sasa Serikali imeshatoa jumla ya Shbil23.8zimetolewa na Serikali kwa wananchi katika kuwawezesha kiuchumi.
Sanjari na hilo amewataka Maafisa maendeleo ya Jamii kutimiza wajibu wao katika kuwasaidia wananchi kuleta maendeleo kwakuanzisha vikundi,viwanda vya Kati ili waweze kujikwamua kiuchumi huku akiwataka kuongeza kasi ya kutumia stadi katika kuielimisha Jamii hasa Kaya maskini ili kujitegemea kwa kubadilisha fikra zao.
Amesema Serikali ya awamu ya tano inatekeleza Miradi mbalimbali ya kisekta na kimkakati ikiwemo reli ya kisasa,Bomba la mafuta,mradi wa kufua umeme na katika kukamilisha miradi hiyo Serikali inahitaji ushiriki wa wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri Gwajima ametoa tamko la kutaka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza kwakuzingata kanuni za afya ikiwemo kunawa mikono huku akimwagiza Mfamasia wa Serikali kutoa maelekezo juu ya matumizi ya tiba za asili kwa wananchi.
Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Nchini(CODEPATA),Wambura Sande amesema mipango ya Chama hicho ni pamoja na kuhamasisha wataalam kujiunga na chama kufanya maandalizi ,kuandaa mpango mkakati wa chama utakaotoa dira ya Chama ambapo pia wamempongeza Rais DK Magufuli kwa utendaji wake wa kazi ikiwemo kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma.
Kauli mbiu ya uchumi wa Kati Serikali imekuwa ikitekeleza mkakati wqkukuza viwanda vikubwa na vya Kati ili kuondokana na dhana ya kuagiza bidhaa toka nje.
Awali akimkaribisha Waziri katika kongamano hilo,Katibu Mkuu, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii,Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsi wazee na watoto,John Jingu amesisitiza suala la maadili kwa maafisa maendeleo ya Jamii.
Kongamano hilo la siku mbili limewashirikisha Maafisa maendeleo ya jamii pamoja na wataalam wa maendeleo ya jamii takribani 200.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *