BARAZA LA MAKANISA YA KIPENTECOSTE (CPCT) IMEANDAA MAOMBI YA SIKU 21KULIOMBEA TAIFA

BARAZA LA MAKANISA YA KIPENTECOSTE (CPCT) IMEANDAA MAOMBI YA SIKU 21KULIOMBEA TAIFA

KATIKA kukabiliana na majanga yanayolikumba taifa la Tanzania na Dunia kwa ujumla,Baraza la Makanisa ya Kipentemost Tanzania( CPCT) limeandaa maombi ya siku ishirini na moja 21. Mbali ya kufanya maombi kwa siku 21 siku ya mwisho ya maombi kunatarajiwa Rais John Magufuli kuwa mgeni rasm katika itimisho ya maombi hayo yanayotaraniwa kufanyika katika ukumbi wa


KATIKA kukabiliana na majanga yanayolikumba taifa la Tanzania na Dunia kwa ujumla,Baraza la Makanisa ya Kipentemost Tanzania( CPCT) limeandaa maombi ya siku ishirini na moja 21.

Mbali ya kufanya maombi kwa siku 21 siku ya mwisho ya maombi kunatarajiwa Rais John Magufuli kuwa mgeni rasm katika itimisho ya maombi hayo yanayotaraniwa kufanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Machi 2 2021 Mwenyekiti wa CPCT  Askofu Peter Konki amesema serikali kuwa katika maombi hayo ya siku 21 yatakuwa yamegawanyika kwa wiki 3 na maombi yatakuwa yakitofautiana.

Amesema wiki ya kwanza yatakuwa maombi kwa ajili ya Toba kwa ajili ya kanisa na Taifa,toba Kwa ajili ya dhambi za viongozi wa Dini wenyewe,toba kwa ajili ya na kanisa kurudi nyuma kiimani,toba kwa ajili ya taifa na wakuu wake na toba kwa ajili ya kuacha kuishi maisha ya haki.

Pia kiongozi huyo amesema wiki ya pili ni maombi ya  uponyaji wa taifa kwa ugonjwa wa Corona,magonjwa ya kisukari,presha,saratani,Tezi Dume,figo,roho ya hofu,njaa,umasikini na nzige walioingia nchini Wiki ya tatu yatakuwa maombi ya shukrani kwa sababu Mungu ametusikia,ametuponya na ameponya taifa letu
Amesema maombi hayo yanatokana na makubaliano ya kikao cha Frebriari 25 milichokubaliana kwa nia moja kufanya maombi ya siku 21 ambayo yatakuwa ya kufunga saa 12 kila siku.

Aidha Askofu Peter Kinki ameeleza kuwa Madhehebu ya kipentekost waliowanachama na wasiowanachama wanatakiwa kushirikiana kwa wale watakaopenda ili kuhakikisha maombi ya kuliombea taifa linaenda vizuri.

Na Packshad Maheneko

DODOMA March 3, 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »