Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amezindua Magari Maalum ya utoaji huduma Tembezi ya Tohara kinga kwa Wanaume.

Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amezindua Magari Maalum ya utoaji huduma Tembezi ya Tohara kinga kwa Wanaume.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezindua Magari matatu Maalum(Mounted Mobile Clinic Vans) kwa ajili ya utoaji wa huduma Tembezi ya Tohara kinga kwa Wanaum katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza,Simiyu na Mara katika Ofisi za OR-TAMISEMI Mtumba Jijini Dodoma Akizindua magari hayo Mh. Jaffo amesema

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezindua Magari matatu Maalum(Mounted Mobile Clinic Vans) kwa ajili ya utoaji wa huduma Tembezi ya Tohara kinga kwa Wanaum katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza,Simiyu na Mara katika Ofisi za OR-TAMISEMI Mtumba Jijini Dodoma

Akizindua magari hayo Mh. Jaffo amesema magari yote matatu yaliyotolewa na Taasisi ya Intra Health International yanathamani ya shilingi bilioni 1.2 na kusema kuwa wale waliopata tohara wana asilimia kubwa ya kujizuia kwa kutopata maambukizi ya ukimwi kwa asilimia 60 na kuwataka waganga wakuu wa mikoa ya kanda ya ziwa washirikiane kwa dhati katika kuhakikisha huduma ya tohara inawafikia wanaume wakubwa na wadogo huku akiwataka kuyatunza magari hayo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya afya ustawi wa jamii na lishe TIMISEMI Ntuli Kapologwe amesema kuwa huduma ya utoaji tohara ni moja ya afua muhimu sana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi Ncnini huku akibainisha kwamba serikali kwa kushirikiana na wadau wa intra health na Afya plus imefanya uwekezaji wa kuwa na watumishi elfu kumi na mbili na mia nane na hamsini na tisa watakao toa huduma katika maeneo hayo.

Naye mkurugenzi mkazi wa shirika la intra health international dr lucy Raymond amesema kuwa shirika limekuwa likitoa huduma ya tohara kwa wanaume wakubwa na wadogo kwa lengo la kuondoa maambukizi ya ukimwi na magonjwa mbalimbali huku akibainisha  wafanyakazi wa kutoa huduma  zaidi ya elfu moja wamepatiwa elimu ya kutoa huduma bora katika mikoa hiyo.

Sambamba na hayo Nuru mpuya mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa shinyanga amesema kuwa wamekuwa wakitoa huduma ya tohara huku akibainisha asilimia kubwa ya wanaume hawajapata tohara tofauti na mikoa mingine ya pwani na kusema huduma ya tohara itawasaidia wanaume wakubwa na wadogo katika mikoa ya kanda yaziwa ili kuondokana na magonjwa mbalimbali.

 KAULI MBIU ni Tohara ya mwanaume “maisha ni sasa,wahi tohara,kuwa msafi,pata kinga.

Na Barnabas kisengi Dodoma.

February 4 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »