Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imezindua mashine maalumu ya kujifukiza.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imezindua mashine maalumu ya kujifukiza.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hii leo imezindua rasmi mashine maalumu ambayo itatumika kutoa huduma za kujifukiza katika hospitali hiyo kuu ya rufaa nchini Tanzania. Mkurugenzi wa Muhimbili Prof Lawrence Maseru ameeleza kuwa, mgonjwa atatumia dakika tano akivuta mvuke wenye mchanganyiko wa dawa asili. Hata hivyo, wataalamu wengi wa afya pamoja na shirika la Afya

Mashine za kujifukizia zafika hopsitali ya Muhimbili

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hii leo imezindua rasmi mashine maalumu ambayo itatumika kutoa huduma za kujifukiza katika hospitali hiyo kuu ya rufaa nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Muhimbili Prof Lawrence Maseru ameeleza kuwa, mgonjwa atatumia dakika tano akivuta mvuke wenye mchanganyiko wa dawa asili.

Hata hivyo, wataalamu wengi wa afya pamoja na shirika la Afya Duniani (WHO) hawakubali matumizi ya mvuke kama tiba ya corona wakionya mvuke unaweza kusababisha madhara makubwa kwenye mfumo wa upuamaji ikiwemo kujaza mapafu maji

Mashine za kujifukizia zafika hopsitali ya Muhimbili

“Hadi sasa hakuna Tiba ya covid hivyo kila dawa inapaswa kujaribiwa matumizi ya miti shamba yameonekana kuwa na faida,” amesema Prof Maseru.

Uongozi wa Muhimbili pia umeeleza kuwa kwa sasa idadi ya wagonjwa wenye ‘matatizo ya upumuaji’ wamepungua hospitalini hapo.

Mashine tatu zaidi zinatarajiwa kufungwa katika hospitali hiyo na nyengine ikitarajiwa kufungwa katika tawi lake la Mloganzila lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mwaka uliopiita rais Magufuli alinukuliwa akisema kwamba wagonja wa virusi vya corona katika hospitali mbali mbali walikuwa wamepungua licha ya serikjali kutotoa takwimu rasmi za viwnago vya maambukizi.

Kiongozi huyo mara kwa mara amesisitiza kwamba watu hawafai kuwa na hofu kuhusu ugonjwa huo.

Serikali ilisitisha utangazaji wa takwimu za ugonjwa huo mara kwa mara mwezi Aprili baada ya rais kulalamika kwamba desturi ya kutangaza idadi ya wagonjwa ilikuwa inaongeza hofu.

Aidha erikali ya Tanzania ilisema ina wasiwasi kwamba kuwafungia watu kwa lengo la kuzuia maambukizi kunaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watu na uchumi, na pia hatua kama hiyo inaweza kuathiri sekta muhimu ya utalii.

Dkt Magufuli pia alitilia shaka usahihi wa matokeo ya vipimo vya corona vilivyokuwa vikifanywa na maabara ya taifa, baada ya sampuli za paipai na mbuzi kuonyesha zilikuwa na virusi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »