Mkurugenzi idara ya Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kati Mwa TanzaniaK[CTF] Mchungaji David Mmbaga amewaasa Wakristo kuacha kukatishwa tamaa kutokana na vikwazo vya dunia kwani vikwazo vina makusudi maalum kwa maisha ya mwanadamu. Mchungaji Mmbaga amebainisha hayo leo Machi,6,2021 katika mahubiri ya ibaada kuu Kanisa la Waadventista Wasabato Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo
Mkurugenzi idara ya Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kati Mwa TanzaniaK[CTF] Mchungaji David Mmbaga amewaasa Wakristo kuacha kukatishwa tamaa kutokana na vikwazo vya dunia kwani vikwazo vina makusudi maalum kwa maisha ya mwanadamu.
Mchungaji Mmbaga amebainisha hayo leo Machi,6,2021 katika mahubiri ya ibaada kuu Kanisa la Waadventista Wasabato Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo amebainisha kuwa vikwazo ni moja ya hatua muhimu kwa maisha ya mwanadamu ili awe kuwa imara zaidi katika imani na maisha ya kawaida ya kila siku.
Katika hatua nyingine, Mhubiri Mkuu katika Sabato ya leo Machi 6,2021 Kanisa la Waadventista Wasabato Kizota jijini Dodoma Dkt.Herry Mhando ametoa hamasa kwa Washiriki kuwa Mstari wa mbele kwa kufanya kazi kwa bidii katika kujikwamua kiuchumi
Aidha,Dkt.Mhando ametumia fursa hiyo kuhimiza washiriki kuwa na desturi ya kusoma Biblia mara kwa mara katika kuwajenga kiroho huku akitoa wito kuendelea kuchangia ili kufanikisha Mahubiri ya Kizota NET Event.
Mahubiri ya Satelite ya Kizota Net Event yanatarajiwa kuanza Mwezi Juni,2021 na yatarushwa na vyombo mbalimbali vya Habari vikiwemo vya Kanisa ambavyo ni Morning Star Radio,Hope Channel Tanzania na mnenaji Mkuu wa Mahubiri hayo ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Union Kuu ya Kusini Mwa Tanzania ,Mchungaji Mark Walwa Malekana.
Na Barnabas Kisengi
Dodoma March 6, 2021
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *