BASKETBALL KARUME CUP KUANZA MACHI 10

BASKETBALL KARUME CUP KUANZA MACHI 10

Kombe la karume Cup kwa mwaka 2021 linatarajiwa kuanza tarehe 10/03/2021 kisiwani Pemba na tarehe 15/03/2021 Unguja. Jumla ya timu 7 za WANAUME kwa Pemba zinatarajiwa kushiriki Kombe hilo na timu 8 za WANAUME NA 4 za WANAWAKE kwa Upande wa Unguja. Pemba watacheza kwa mtindo wa ligi na timu mbili za kwanza zitaingia hatua

Kombe la karume Cup kwa mwaka 2021 linatarajiwa kuanza tarehe 10/03/2021 kisiwani Pemba na tarehe 15/03/2021 Unguja.

Jumla ya timu 7 za WANAUME kwa Pemba zinatarajiwa kushiriki Kombe hilo na timu 8 za WANAUME NA 4 za WANAWAKE kwa Upande wa Unguja.

Pemba watacheza kwa mtindo wa ligi na timu mbili za kwanza zitaingia hatua ya nusu fainal na Unguja watacheza kwa group 2 na timu 2 zakila group watacheza hatua ya mtoani nakupatikana timu 2 zitakazoingia hatua ya nusu fainali.

Nusu fainal zitachezwa Unguja na timu mbili za Pemba zitasafiri kuja Unguja na nusu fainal yakwanza itakua ni kati ya MSHINDI WA kwanza Unguja na MSHINDI WA pili Pemba na nusu fainal ya pili itakua ni MSHINDI WA kwanza Pemba na MSHINDI WA pili Unguja. Na washindi wa nusu fainal hizo watacheza fainal na waliopoteza watacheza kutafuta MSHINDI WA tatu.

Kwa upande wawanawake mtindo wa ligi utatumika na atakaeshinda michezo mingi ndio atakua bingwa.

TIMU ZA Pemba ni kama zifuatazo

1.Clikers 2. Tornado 3. Mkoani bulls 4.majenzi 5.kichungwani blezz 6.dolphine na 7. California.

Unguja WANAUME.

  1. Stone Town 2. New West 3. Usolo 4. Polisi 5 NYUKI 6. A. Magic 7.Milenium na 8 J. K. U

WANAWAKE Unguja

1.J.K.U 2. NEW WEST 3.K.V.Z NA 4 ZIMAMOTO

GROUP A.

  1. A. MAGIG 2.MILLENIUM 3.USOLO NA STONE TOWN

GROUP B.

1.POLISI
2.NEW WEST

  1. NYUKI
  2. J. K. U

Kombe hili la karume Cup linafanyika chini ya udhamini Mkubwa wa familia ya Rais wa kwanza wa Zanzibar na gemedari wa mapinduzi matukufu ya Zanzibar shehe Abeid Amani karume chini ya uongoz na mdhamini Mkuu mr. Ahmed karume.

Lengo KUU la Kombe hili nikumkumbuka na kumuenzi pamoja na kuyaenzi yale yote mazur yaliyofanywa na Rais Abeid Aman Karume.

TIMU zote shiriki zitapatiwa maji katoon 2 ya letter 1.5 kwa kila mchezo, kwaiyo mda wote wa mchezo timu zitakua na maji ya kutosha.

Zawadi.

Mhindi wa kwanza kwa WANAUME NA WANAWAKE watapat Tzsh laki tano (500,000) Kombe, jezi seti moja na mpira mmoja.

MSHINDI WA pili wakiume na wakike wataipata laki tatu (300,000/) Kombe, jezi seti moja na mpira mmoja.

MSHINDI WA tatu wakike na wakiume watapata laki moja na nusu (150,000) mpira na jezi seti moja.

TIMU zote zilizoshiriki zitapata seti moja ya jezi na mpira mmoja mmoja.

Huu ni mwaka wa 19 sasa tangu Kombe hili lillipoanzishwa na karume Cup huchezwa kila mwaka visiwani Zanzibar.

Chama kinatoa shukurani za dhati kwa familia ya shehe Abeid Amani karume hususan Mwenyekiti wa karume Cup na mdhamini Mkuu wa Kombe hili Nd. Ahmed karume kwa moyo wake wakujitolea na mashirikiano mkubwa anayotupatia katika kulisukuma mbele gurudumu letu la basketball.

Shukurani pia kwa Mama shadya Karume Mlezi wa Chama cha basketball Zanzibar na mwenyekiti wa Taasisi ya Zayadesa kwa mashirikiano mkubwa aliyotupatia tangu kuanza kwa Kombe hili miaka 18 iliyopiata hadi Leo hii.

Ahsanteni

Rashid hamza khamis

Makamo Mwenyekiti BAZA

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »